Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Fuliza Kushikilia kwa Imara Kile Ulicho Nacho”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na kwa malaika wa kundi katika Filadelfia andika: Hivi ndivyo vitu ambavyo husema yeye ambaye ni mtakatifu, aliye wa kweli, ambaye ana ufunguo wa Daudi, ambaye hufungua hivi kwamba hakuna mmoja ambaye atafunga, na hufunga hivi kwamba hakuna mmoja ambaye hufungua.”—Ufunuo 3:7, NW.

  • “Fuliza Kushikilia kwa Imara Kile Ulicho Nacho”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Ufunguo wa Daudi”

      4, 5. “Ufunguo wa Daudi” ulishirikishwa na agano gani?

      4 Yesu ana “ufunguo wa Daudi.” Akiutumia, yeye “hufungua hivi kwamba hakuna mmoja ambaye atafunga, na hufunga hivi kwamba hakuna mmoja ambaye hufungua.” Ni nini huu “ufunguo wa Daudi”?

      5 Yehova alifanya agano la Ufalme wa milele na Mfalme Daudi wa Israeli. (Zaburi 89:1-4, 34-37) Nyumba ya Daudi ilitawala kutoka kiti cha ufalme cha Yehova katika Yerusalemu tangu 1070 mpaka 607 K.W.K., lakini ndipo hukumu ya Mungu ikafikilizwa juu ya ufalme huo kwa sababu uligeuka ukawa mbovu. Hivyo Yehova akaanza kutimiza unabii wake kwenye Ezekieli 21:27, NW: “Magofu, magofu, magofu mimi nitalifanya liwe [Yerusalemu la kidunia]. Na kwa habari ya hii pia, hiyo [fimbo ya umaliki katika nasaba ya Daudi] hakika haitakuwa ya mwingine mpaka ajapo ambaye ana haki halali, nami lazima nimpe hiyo.”

      6, 7. Ni wakati gani na jinsi gani yule aliye na “haki halali” angetokea?

      6 Ni wakati gani na jinsi gani huyu mmoja mwenye “haki halali” angetokea? Ni jinsi gani yeye angepewa fimbo ya ufalme wa Daudi?

      7 Yapata miaka 600 baadaye, mzao wa Mfalme Daudi, yule msichana Myahudi Mariamu, akapata mimba kwa roho takatifu. Mungu alimtuma malaika Gabrieli kumwambia Mariamu kwamba yeye angepata mwana, ambaye angeitwa Yesu. Gabrieli aliongeza hivi: “Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana [Yehova, NW] Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.”—Luka 1:31-33.

      8. Yesu alijithibitishaje kuwa anastahili kurithi ufalme wa Kidaudi?

      8 Wakati Yesu alipobatizwa katika mto Yordani na kupakwa mafuta kwa roho takatifu katika 29 W.K., akawa Mfalme-Mchaguliwa katika nasaba ya Daudi. Yeye alionyesha bidii iliyo kielelezo chema katika kuhubiri habari njema za Ufalme na akawapa utume wanafunzi wake wahubiri vivyo hivyo. (Mathayo 4:23; 10:7, 11) Yesu alijinyenyekeza, hata mpaka kifo kwenye nguzo ya mateso, akijithibitisha hivyo kustahili kabisa kurithi ule umaliki wa Kidaudi. Yehova alimfufua Yesu akiwa roho asiyeweza kufa akamkweza kwenye mkono wa kulia Wake katika mbingu. Huko alirithi haki zote za ufalme wa Kidaudi. Wakati uwadiapo Yesu angetumia haki yake ‘aende akitiisha katikati ya adui zake.’—Zaburi 110:1, 2, NW; Wafilipi 2:8, 9; Waebrania 10:13, 14.

      9. Ni jinsi gani Yesu anatumia ufunguo wa Daudi kufungua na kufunga?

      9 Kwa wakati uliopo Yesu angetumia ule ufunguo wa Daudi, akifungua nafasi na mapendeleo yanayohusiana na Ufalme wa Mungu. Kupitia Yesu, Yehova angekomboa Wakristo wapakwa-mafuta duniani “kutoka mamlaka ya lile giza,” na kuwahamisha awaingize “ndani ya ufalme wa Mwana wa upendo wake.” (Wakolosai 1:13, 14, NW) Ufunguo ule ungetumiwa pia kuzuia wasipate mapendeleo hayo wowote ambao wangethibitika kuwa wasioaminika. (2 Timotheo 2:12, 13) Kwa kuwa mrithi huyu wa kudumu wa ufalme wa Daudi ana utegemezo wa Yehova, hakuna kiumbe anayeweza kumzuia asitimize wajibu huo ulio mwingi.—Linga Mathayo 28:18-20.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki