Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Uweke Pesa Akiba Badala ya Kuzitumia?
    Amkeni!—2011 | Septemba
    • Deni la Lazima

      Ni watu wachache wanaoweza kulipa pesa taslimu kwa ajili ya nyumba wanayonunua. Kwa hiyo, wengi huchukua mkopo kwenye benki ili kununua nyumba. Kiasi wanacholipa kila mwezi ili kurudisha pesa hizo huonwa ni kana kwamba wanalipa kodi ya nyumba. Lakini baada ya kulipa mkopo huo kwa muda mrefu, wanamiliki nyumba hiyo!

      Pia watu wengi huona kuwa inafaa kuchukua mkopo ili kununua gari ambalo halitumii petroli nyingi. Wanapolipa mkopo huo upesi iwezekanavyo, gari hilo huwa na faida, na hiyo ni njia nyingine ya kuokoa pesa.b Wengine wameona ni jambo la hekima kununua gari la mtumba lililo katika hali nzuri na ambalo halijatumiwa sana. Wengine huokoa pesa kwa kutumia usafiri wa umma au hata kuendesha baiskeli.

  • Kwa Nini Uweke Pesa Akiba Badala ya Kuzitumia?
    Amkeni!—2011 | Septemba
    • b Kumbuka kwamba ukipoteza kazi yako na ushindwe kulipia mkopo, huenda ukapoteza nyumba au gari lako na pesa zote ulizokuwa umelipa kufikia wakati huo. Ingawa hivyo, wengi huamua kuwa na bima ya kuzuia hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki