Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Uwakabidhi Wengine Kazi—Unaweza Kufanya Hivyo Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Juni 15
    • Kwa Nini Uwakabidhi Wengine Kazi—Unaweza Kufanya Hivyo Jinsi Gani?

      YEHOVA alianza kuwakabidhi wengine madaraka au kazi muda mrefu kabla ya Dunia kuumbwa. Alimuumba Mwana wake mzaliwa-pekee kisha akaumba ulimwengu wote akimtumia Mwana huyo akiwa “stadi wa kazi.” (Met. 8:22, 23, 30; Yoh. 1:3) Mungu alipowaumba wenzi wawili wa kwanza, aliwaambia ‘wajaze dunia na kuitiisha.’ (Mwa. 1:28) Muumba aliwapa wanadamu kazi ya kupanua Paradiso ya Edeni mpaka ijaze dunia yote. Ndiyo, tangu mwanzo, tengenezo la Yehova limekuwa likiwakabidhi wengine kazi.

  • Kwa Nini Uwakabidhi Wengine Kazi—Unaweza Kufanya Hivyo Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Juni 15
    • Kwa Nini Uwakabidhi Wengine Kazi?

      Fikiria jinsi Yehova alivyomuumba Mwana wake mzaliwa-pekee na kushiriki naye katika kazi iliyobaki ya uumbaji. Ndiyo, “kwa njia yake vitu vingine vyote viliumbwa mbinguni na duniani, vitu vinavyoonekana na vitu visivyoonekana.” (Kol. 1:16) Muumba angefanya kazi yote peke yake, lakini alitaka Mwana wake apate pia shangwe iliyotokana na kutimiza kazi hiyo nzuri. (Met. 8:31) Hilo lilimsaidia Mwana wake kujifunza mengi zaidi kuhusu sifa za Mungu. Kwa njia fulani, Baba alitumia nafasi hiyo kumzoeza Mwana wake mzaliwa-pekee.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki