Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unawaogopa Wafu?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Januari 1
    • Agboola pia alitambua kwamba alihitaji kuacha kabisa mazoea ya kuwasiliana na pepo. Aliteketeza vitu vyote alivyotumia katika uchawi. (Matendo 19:19) Watu fulani katika eneo lake walimwonya kwamba roho waovu wangekasirika. Lakini Agboola hakuogopa. Alifuata shauri linalopatikana katika Andiko la Waefeso 6:11, 12: “Vaeni mavazi kamili ya silaha kutoka kwa Mungu . . . kwa sababu tuna kushindana mweleka . . . juu ya majeshi ya roho waovu.” Mavazi hayo ya silaha ya kiroho yanatia ndani kweli, uadilifu, habari njema ya amani, imani, na upanga wa roho, yaani, Neno la Mungu. Silaha hizo zinatoka kwa Mungu na ni zenye nguvu!

  • Je, Unawaogopa Wafu?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Januari 1
    • Ikiwa unawasiliana na pepo, acha mara moja. Jilinde dhidi ya roho waovu kwa kuvaa “mavazi kamili ya silaha kutoka kwa Mungu.” (Waefeso 6:11) Mashahidi wa Yehova watafurahi kukusaidia. Wao wanajifunza na watu Biblia wakitumia kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa?a

      Agboola hawaogopi wafu tena, na amejifunza jinsi ya kupinga roho waovu. Anasema: “Sijui ni nani aliyesababisha kifo cha wana wangu watatu. Lakini tangu nianze kumtumikia Yehova, nimepata watoto wengine saba. Hakuna yeyote kutoka makao ya roho ambaye amewadhuru.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki