-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
na mkia wake huburuta theluthi ya nyota za mbingu, na ukazivurumisha chini kwenye dunia. Na drakoni akafuliza kusimama mbele ya mwanamke ambaye alikuwa karibu kuzaa, kwamba, wakati ambapo yeye angezaa, apate kumeza mtoto wake.”—Ufunuo 12:3, 4, NW.
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
9. Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba mkia wa huyo drakoni “huburuta theluthi ya nyota za mbingu” kuziangusha chini kwenye dunia?
9 Pia drakoni ana mamlaka katika milki ya kiroho. Kwa mkia wake, yeye “huburuta theluthi ya nyota za mbingu.” Nyota zaweza kuwakilisha malaika. (Ayubu 38:7) Mtajo “theluthi” ungekazia kwamba idadi kubwa sana ya malaika wameongozwa vibaya na Shetani. Mara hawa walipokuja chini ya udhibiti wake, hawakuwa na njia ya kuponyoka. Hawangeweza kurudi kwenye tengenezo takatifu la Mungu. Wakaja kuwa roho waovu, wakawa kana kwamba wameburutwa na Shetani, mfalme, au mtawala wao. (Mathayo 12:24)
-