-
Kutoka kwa Wasomaji WetuAmkeni!—2004 | Oktoba 8
-
-
Dada yangu ana ugonjwa wa kushuka moyo. Nililia niliposoma makala hizo kwani nilitambua kwamba nilikuwa nikiongea kuhusu hali yake bila kumwelewa. Sasa ninafahamu kwamba badala ya kuchoshwa na dada yangu, ninapaswa kujitahidi kwa subira kuelewa hali yake.
D. P., Marekani
-
-
Kutoka kwa Wasomaji WetuAmkeni!—2004 | Oktoba 8
-
-
Nina umri wa miaka 13. Mara nyingi mimi hutamani kufa. Gazeti la Amkeni! limenisaidia sana kukabili hisia hizo. Sasa najua kwamba Yehova anatujali na kwamba yeye hutusikiliza!
M. S., Marekani
Nimekuwa nikifikiri kwamba kushuka moyo husababishwa na ubinafsi, na kwamba mtu anahitaji tu kuacha kushuka moyo. Lakini niliposoma makala hizo, nilitambua kwamba mimi ndiye niliyekuwa na ubinafsi kwa kutowajali wengine.
R. N., Marekani
Asanteni sana kwa makala hizo zilizoandikwa vizuri. Zina habari zinazoweza kutumiwa katika matibabu ya ugonjwa huo. Niko katika chuo kikuu na ninasomea jinsi ya kutoa ushauri wa kisaikolojia, nami nitawapa wateja wangu habari hiyo.
P. Y., Marekani
Nimekuwa nikipambana na ugonjwa wa kushuka moyo kwa zaidi ya miaka kumi. Makala hizo zilionyesha umuhimu wa mtu kuandika mambo anayofanya, nami nitafanya hivyo. Ninapokosa kufika mikutanoni, rafiki yangu ambaye ni Mkristo hunisaidia sana kwa kurekodi habari inayozungumziwa huko kwa ajili yangu.
M. S., Japani
-
-
Kutoka kwa Wasomaji WetuAmkeni!—2004 | Oktoba 8
-
-
Mimi ni mzee wa miaka 68, na nimekuwa na ugonjwa wa kushuka moyo kwa miaka kumi hivi. Wazee Wakristo pia wanahitaji msaada, na baadhi yao hushuka moyo sana. Niliguswa moyo sana kusoma kuhusu jinsi watu wengine wanavyokabiliana na ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika.
B. A., Marekani
Habari iliyo katika makala hizo ilinichochea kutafuta matibabu. Imemsaidia pia mke wangu kushughulika vizuri zaidi na ugonjwa wangu wa kushuka moyo. Nyakati zote mimi hufurahi kuona jinsi makala zenu zilivyo sahihi na za wakati unaofaa.
C. B., Ujerumani
Iligunduliwa kwamba nina ugonjwa wa kushuka moyo miezi mitatu kabla ya kusoma mfululizo huu. Itikio langu la kwanza ni sawa na lile lililoonyeshwa katika mfululizo huo, yaani kushtuka na kuogopa kumwambia mtu mwingine juu ya hali yangu. Makala zenu zilinisaidia kujua kwamba wengine wanaelewa hali yangu, nami sihisi upweke.
A. G., Austria
-
-
Kutoka kwa Wasomaji WetuAmkeni!—2004 | Oktoba 8
-
-
Nimekuwa nikilia kila mara mtu anaponiambia kwamba tukiwa Wakristo hatuwezi kushuka moyo. Hata hivyo, makala hizo zimenisaidia, nami nimefarijiwa kujua kwamba kuna wengine pia wanaokabili tatizo hilo.
P. B., Uingereza
-