Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Akili Zilizovurugika
    Amkeni!—2004 | Januari 8
    • Akili Zilizovurugika

      NICOLE amekuwa akishuka moyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 14. Hata hivyo, alipokuwa na umri wa miaka 16, alianza kuhisi tofauti—alisisimuka kupita kiasi na kuhisi ana nguvu nyingi mno. Aliwaza sana, alisema mambo yasiyoeleweka, alikosa usingizi na kushuku kwamba marafiki wake wanamtumia ili kujifaidi. Kisha, Nicole alidai kwamba angeweza kubadilisha rangi ya vitu. Hapo ndipo mama yake alipotambua kwamba Nicole anahitaji kumwona daktari, kwa hiyo akampeleka hospitalini. Baada ya kumchunguza, madaktari wakagundua kwamba Nicole ana ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika.a

      Kama Nicole, mamilioni ya watu ulimwenguni pote wana ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika au ugonjwa wa kushuka moyo. Magonjwa hayo yanaweza kusababisha madhara makubwa mno. Steven anayeugua ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika anasema: “Nilifadhaika kwa miaka mingi, nilishuka moyo na wakati mwingine nikasisimuka kupita kiasi. Matibabu yalisaidia, lakini bado nilifadhaika.”

      Ni nini kinachosababisha magonjwa ya kihisia? Watu walioshuka moyo au wenye ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika hukabili magumu gani? Wagonjwa na wale wanaowatunza wanaweza kusaidiwaje?

      [Maelezo ya Chini]

      a Baadhi ya dalili zilizotajwa zinaweza pia kuwa dalili za ugonjwa wa akili, matumizi ya dawa za kulevya, au hata mabadiliko yanayotukia wakati wa kubalehe. Ugonjwa unaweza kutambuliwa tu baada ya kuchunguzwa kikamili na mtaalamu.

  • Kuishi na Ugonjwa wa Kihisia
    Amkeni!—2004 | Januari 8
    • Katika miaka ya karibuni, watu wengi zaidi wameufahamu ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika. Dalili za ugonjwa huo zinatia ndani kushuka moyo na baadaye kusisimuka kupita kiasi. Kitabu kimoja kilichochapishwa hivi majuzi na Chama cha Kitiba cha Marekani kinasema kwamba “mtu anaposhuka moyo, anaweza kutaka kujiua. Wakati mtu amesisimuka sana, anaweza kushindwa kuamua mambo vizuri na kufanya mambo hatari bila kutambua.”

      Inakadiriwa kwamba asilimia 2 ya watu nchini Marekani wanaugua ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika, hivyo kuna mamilioni ya watu wanaougua ugonjwa huo nchini humo pekee. Hata hivyo, takwimu hazionyeshi msononeko ambao wagonjwa hao hupata.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki