Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2004 | Oktoba 8
    • Ilipogunduliwa kwamba nina ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika, nilihisi kuwa maisha yangu yameharibika. Nililia sana, lakini pia nilisali kwa Yehova. Sala yangu ilijibiwa juma hili nilipopokea gazeti la Amkeni! linalozungumzia magonjwa ya kihisia. Ni kana kwamba Yehova ananipenda mimi binafsi. Makala hizo zimeniimarisha nisonge mbele.

      R. T., Kanada

      Miaka mitatu iliyopita iligunduliwa kwamba mto- to wetu mwenye umri wa miaka 12 alikuwa na ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika. Mara nyingi yeye huhisi kwamba hakuna mtu anayefahamu hali yake na kwamba Yehova hamjali. Tulimpa gazeti hilo, naye akalisoma mara moja. Alilia huku akisema hivi: “Mama, kuna watu wanaoelewa. Yehova pia anaelewa hali yangu.” Daktari anayemtibu alifurahia kupokea gazeti hilo, nami nikafurahia kuzungumza naye kuhusu Biblia.

      L. P., Marekani

      Nilimsihi Yehova katika sala na kumwomba makala kuhusu ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika. Nimepokea toleo la Amkeni! la Januari 8, 2004, miezi miwili tu tangu nilipotoa sala yangu. Madokezo mliyotoa yamenisaidia kumtumikia Yehova zaidi.

      M. S., Mexico

      Nilitumia habari hiyo ya mfululizo kufanya kazi fulani chuoni. Msimamizi wa idara ya wenye mahitaji ya pekee, aliomba nakala ya gazeti hilo ili alitumie kuwafundisha wafanyakazi kuhusu ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika. Endeleeni kuchapisha makala hizo bora. Zinanufaisha watu wengi.

      K. R., Marekani

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2004 | Oktoba 8
    • Baba yangu amekuwa na ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika tangu nilipokuwa mchanga. Aliposisimuka kupita kiasi nilichukizwa naye, ingawa nilijua kwamba alikuwa mgonjwa. Lakini niliposoma mfululizo huo, nilifahamu mambo aliyokuwa akikabili. Nililia nilipokuwa nikisoma makala hizo. Nitazungumza naye nitakapoenda nyumbani. Nitajaribu niwezavyo kuvumilia hali yake.

      S. S., Japani

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki