-
Misiba ya Asili—Jinsi Wanadamu Wanavyochangia Kuongezeka KwakeAmkeni!—2005 | Julai 22
-
-
Misiba ya Asili—Jinsi Wanadamu Wanavyochangia Kuongezeka Kwake
GARI linapotunzwa vizuri, linaweza kusafirisha watu kwa usalama. Lakini gari hilo likitumiwa vibaya na kutotunzwa linaweza kuwa hatari. Kwa njia fulani, tunaweza kusema hivyo kuhusu dunia.
Wanasayansi kadhaa wanaona kwamba mabadiliko yanayosababishwa na wanadamu katika angahewa na bahari yamechangia kuongezeka kwa misiba ya asili iliyo mibaya zaidi na kufanya dunia iwe mahali hatari. Na huenda mambo yakawa mabaya wakati ujao. Tahariri katika gazeti Science ilisema hivi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa: “Hatujui mambo tunayofanya katika sayari pekee ambayo wanadamu wanaweza kuishi yatakuwa na matokeo gani.”
-
-
Misiba ya Asili—Jinsi Wanadamu Wanavyochangia Kuongezeka KwakeAmkeni!—2005 | Julai 22
-
-
Kama ilivyotajwa katika makala iliyotangulia, kumekuwa na dhoruba nyingi kubwa katika miaka ya karibuni. Wanasayansi wanachunguza ikiwa dhoruba hizo zinahusiana na ongezeko la joto duniani, ambalo huenda likawa linafanya dhoruba ziwe na nguvu nyingi zaidi. Hata hivyo, huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakawa dalili moja tu ya kuongezeka kwa joto duniani. Huenda matokeo mengine yenye kudhuru yakawa yanaonekana.
Kuongezeka kwa Maji Baharini na Ukataji-Miti
Kulingana na tahariri katika jarida Science, “maji baharini yamepanda kwa sentimeta 10 hadi 20 [inchi nne hadi nane] katika karne iliyopita, na huenda yakapanda zaidi.” Jambo hilo linaweza kuhusianaje na kuongezeka kwa joto duniani? Watafiti wanasema huenda kukawa na njia mbili. Njia moja ni uwezekano wa barafu kuyeyuka na kuongeza maji baharini. Njia nyingine ni kuongezeka kwa joto baharini ambalo hufanya maji yaongezeke.
Huenda tayari visiwa vidogo vya Tuvalu katika Bahari ya Pasifiki vinapatwa na athari za kupanda kwa maji baharini. Gazeti Smithsonian linasema kuwa vipimo vilivyokusanywa kwenye kisiwa cha matumbawe cha Funafuti vinaonyesha kwamba maji baharini yamepanda “kwa wastani wa milimeta 5.6 kila mwaka katika miaka kumi iliyopita.”
Katika sehemu nyingi za ulimwengu, kuongezeka kwa idadi ya watu kumefanya miji ipanuliwe, mitaa ya mabanda iongezeke, na kuharibiwa kwa mazingira. Huenda mambo hayo yakafanya misiba ya asili iwe mibaya zaidi. Fikiria mifano kadhaa.
Haiti, ni kisiwa chenye watu wengi na misitu yake imekatwa kwa muda mrefu. Ripoti moja ya habari ya karibuni ilisema kwamba hata ingawa matatizo ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii nchini Haiti ni mabaya, ukataji-miti ndio unaohatarisha maisha ya watu zaidi nchini humo. Hatari hiyo ilionekana wazi mnamo 2004, mvua za mafuriko ziliposababisha maporomoko ya matope na kuua maelfu ya watu.
Gazeti Time la Asia linataja “ongezeko la joto duniani, mabwawa, ukataji-miti na kilimo cha kufyeka na kuchoma miti na mimea” kuwa sababu zinazozidisha misiba ya asili ambayo imekumba Asia Kusini. Pia ukataji-miti unaweza kufanya ukame uwe mbaya zaidi kwa kufanya udongo ukauke haraka zaidi. Katika miaka ya karibuni, ukame nchini Indonesia na Brazili umetokeza mioto mikubwa katika misitu yenye miti mibichi ambayo kwa kawaida ni vigumu kuteketea.
-
-
Misiba ya Asili—Jinsi Wanadamu Wanavyochangia Kuongezeka KwakeAmkeni!—2005 | Julai 22
-
-
Hata hivyo, wanadamu pia walichangia kwa kiasi fulani madhara yaliyosababishwa na msiba huo. Kisababishi kimoja ni idadi kubwa ya watu wanaoishi katika maeneo hatari. Mwandishi Andrew Robinson anasema: “Karibu nusu ya majiji makubwa ulimwenguni yako katika sehemu ambazo matetemeko yanaweza kutokea.” Kisababishi kingine ni majengo, yaani, vifaa vya ujenzi vilivyotumiwa na ubora wa jengo. Msemo, “Matetemeko ya nchi hayaui watu; watu huuawa na majengo,” umethibitika kuwa kweli mara nyingi. Lakini watu wanaweza kufanya nini ikiwa wao ni maskini sana wasiweze kujenga nyumba zinazoweza kuhimili matetemeko ya nchi?
-
-
Misiba ya Asili—Jinsi Wanadamu Wanavyochangia Kuongezeka KwakeAmkeni!—2005 | Julai 22
-
-
Kwa kupendeza, mara nyingi volkano hutoa dalili mapema kabla ya kulipuka. Ndivyo Mlima Pelée, kwenye kisiwa cha Karibea cha Martinique, ulivyofanya mwaka wa 1902. Hata hivyo, uchaguzi ulikuwa ukikaribia katika jiji la St. Pierre lililokuwa karibu na mlima huo, nao wanasiasa waliwatia watu moyo wasihame licha ya majivu, ugonjwa na woga uliotanda jijini humo. Hata maduka mengi yalikuwa yamefungwa kwa siku nyingi!
Mei 8 ilikuwa siku ya kusherehekea kupaa kwa Yesu Kristo mbinguni, na watu wengi walienda kwenye kanisa Katoliki ili kuomba wakombolewe kutokana na volkano hiyo. Asubuhi hiyo, dakika chache kabla ya saa mbili, Mlima Pelée ulilipuka na kutupa angani majivu, vipande vya lava na glasi, mawe mepesi ya volkano, na gesi moto sana iliyokuwa na joto la kati ya nyuzi 200 hadi 500 Selsiasi. Mchanganyiko huo hatari ulipotiririka chini ulifunika jiji hilo na kuwaua watu karibu 30,000, ukayeyusha kengele ya kanisa na kuteketeza meli zilizokuwa bandarini. Mlipuko huo ndio uliokuwa mbaya zaidi katika karne ya 20. Lakini haungekuwa mbaya hivyo ikiwa watu wangetii maonyo.
Je, Misiba ya Asili Itaongezeka?
Katika ripoti yao ya World Disasters Report 2004, Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu, linasema kwamba katika miaka kumi iliyopita, misiba inayosababishwa na vitu vya asili na hali ya hewa imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60. Ripoti hiyo iliyochapishwa kabla ya msiba wa tsunami uliotokea Desemba 26 katika Bahari ya Hindi, inasema: “Hilo linaonyesha jinsi mambo yatakavyokuwa kwa muda mrefu.” Bila shaka, idadi ya watu katika maeneo hatari ikiendelea kuongezeka na misitu iendelee kukatwa, hakuna matumaini.
Isitoshe, nchi nyingi zilizoendelea kiviwanda zinazidi kutokeza gesi zinazoongeza joto katika angahewa la dunia. Kulingana na tahariri katika jarida Science, kusitasita kupunguza gesi zinazochafua hewa “ni sawa na kutotibu ambukizo linapoanza: Kufanya hivyo kutatokeza gharama kubwa baadaye.” Ikitaja gharama hizo, ripoti moja ya Kanada ya kupunguza misiba ilisema: “Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusemwa kuwa suala kubwa zaidi la kimazingira ambalo limewahi kushughulikiwa na jumuiya ya kimataifa.”
Hata hivyo, sasa hivi jumuiya ya kimataifa haiwezi kukubaliana kuwa utendaji wa wanadamu unachangia kuongezeka kwa joto duniani, na hata haiwezi kukubaliana na jinsi ya kusuluhisha jambo hilo. Hali hiyo inatukumbusha ukweli huu wa Biblia: “Mwanadamu . . .
-