Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Mungu Anapaswa Kulaumiwa?
    Amkeni!—2007 | Septemba
    • Jifunze Kutambua Dalili

      Mwanzoni lazima tukubali kwamba misiba ya asili inaweza kutokea bila onyo. Mhubiri 9:11 inasema: “Wakati na tukio lisilotazamiwa [hutupata sote].” Lakini mara nyingi, kunakuwa na maonyo, ya kiasili au kutoka kwa wenye mamlaka, kwamba hatari inakaribia. Hivyo, watu wanapotambua dalili, wanaweza kupata nafasi ya kuokoka.

      Tsunami ilipopiga kisiwa cha Simeulue huko Indonesia, mnamo 2004, ni watu saba tu waliokufa kati ya maelfu ya watu. Kwa sababu wakazi wa eneo hilo wanajua kwamba maji yanaposonga mbali sana kutoka ufuoni kwa njia isiyo ya kawaida, inamaanisha kwamba tsunami iko karibu kutokea, wengi wao walikimbia walipoona hilo likitukia. Vivyo hivyo, watu wamepona dhoruba kali na milipuko ya volkano kwa kutii maonyo. Kwa sababu nyakati nyingine maonyo ya kiasili huwa yameanza mapema kabla ya maonyo kutoka kwa wenye mamlaka, ni jambo la hekima kufahamiana na yote, hasa ikiwa unaishi katika eneo ambalo misiba hutokea sana.

      Hata hivyo, inasikitisha kwamba “watu wana mwelekeo wa kupuuza hatari hata wakati inapoonekana wazi,” anasema mtaalamu wa masuala ya volkano. Hilo ni kweli hasa kunapokuwa na maonyo ya uongo au mahali ambapo misiba ya kiasili ilitokea zamani sana. Wakati mwingine watu hawapendi kuacha mali zao za kimwili, hata inapokuwa wazi kwamba msiba utatokea.

  • Je, Mungu Anapaswa Kulaumiwa?
    Amkeni!—2007 | Septemba
    • ◼ Sikiliza maonyo yanayotolewa na serikali. ‘Jitiishe kwa mamlaka zilizo kubwa.’ (Waroma 13:1) Wenye mamlaka wanapotoa amri ya kuhama au ya kufuata hatua fulani za kiusalama, ni vizuri kutii. Tadashi alikaa mbali na eneo la hatari ili atii amri ya kuhama na hivyo akaepuka kujeruhiwa au kufa kutokana na matetemeko madogo baada ya tetemeko kubwa kutokea.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki