-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
Kuzingatia hekima kwahusisha kujifunza ufahamu na uelewevu. Kwa mujibu wa Webster’s Revised Unabridged Dictionary, ufahamu ni “nguvu au uwezo unaowezesha akili kupambanua mambo.” Ufahamu wa kimungu ni uwezo wa kupambanua mema na mabaya, kisha kuchagua mwenendo ufaao. ‘Tusipoielekeza mioyo’ yetu ipate ufahamu au tusipokuwa na hamu ya kujipatia ufahamu huo, tunawezaje kukaa katika ‘barabara iongozayo kuingia katika uhai’? (Mathayo 7:14; linganisha Kumbukumbu la Torati 30:19, 20.) Kujifunza na kutumia Neno la Mungu hutupa ufahamu.
-
-
“Bwana Huwapa Watu Hekima”Mnara wa Mlinzi—1999 | Novemba 15
-
-
Kupata hekima na ufahamu huhusisha kutafakari jinsi tuwezavyo kutumia yale tunayojifunza katika kutatua matatizo na kufanya maamuzi.
-