-
Jinsi ya Kukabiliana na Kuvunjika MoyoMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
-
-
● Baruku alipiga kite hivi: “Ole wangu! kwa maana BWANA ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha.”—Yeremia 45:3.
-
-
Jinsi ya Kukabiliana na Kuvunjika MoyoMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
-
-
Baruku, mwandishi wa nabii Yeremia, alilalamika kwa sababu ya mikazo iliyosababishwa na kazi yake. Hata hivyo, kwa fadhili Yehova alimsaidia Baruku aone tatizo lake. “Je, unajitafutia mambo makuu? usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema BWANA; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.”—Yeremia 45:2-5.
Yehova alieleza wazi kwamba kuvunjika moyo kwa Baruku kulisababishwa na ubinafsi wake mwenyewe. Baruku hakuweza kufurahia kazi ambayo alipewa na Mungu, huku akijitafutia mambo makuu. Yamkini hata wewe utapata kwamba njia bora ya kushinda kuvunjika moyo ni kuepuka kuvutiwa na mambo mengi. Na badala yake kujipatia amani ya akili ambayo hutokana na uradhi wa kimungu.—Wafilipi 4:6, 7.
-