-
Je, Kuunganisha Ulimwengu Kutatatua Matatizo Yetu Kweli?Amkeni!—2002 | Mei 22
-
-
Je, Suluhisho Ni Kuunganisha Ulimwengu?
Sawa na miradi mingi ya wanadamu, utandaridhi umeleta faida na hasara. Umewawezesha watu fulani kufaidika kiuchumi, na kuleta maendeleo katika mawasiliano ya ulimwenguni pote. Hata hivyo, unawafaidi matajiri na watu wenye uwezo kuliko maskini. Wahalifu wametumia faida za utandaridhi vizuri kuliko serikali mbalimbali. Na virusi vinavyosababisha magonjwa vimeenea kwa sababu ya utandaridhi.—Ona masanduku kwenye ukurasa wa 8 na 9.
Utandaridhi umeongeza sana matatizo ulimwenguni. Badala ya kusuluhisha matatizo hayo, utandaridhi umechangia matatizo. Migawanyiko na mfadhaiko umeongezeka katika jamii.
-
-
Njia ya Kuunganisha Ulimwengu Ambayo ItakufaidiAmkeni!—2002 | Mei 22
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 12]
WAMEUNGANISHWA LAKINI BADO WAMEGAWANYIKA
Ijapokuwa tekinolojia imewaunganisha watu ulimwenguni pote, bado kuna migawanyiko. Televisheni, simu za mkononi, na Internet zimewawezesha watu kuwasiliana lakini hazijawawezesha kuwa kitu kimoja. Biashara ya ulimwenguni pote na kumalizika kwa uhasama kati ya mataifa yenye uwezo kumepunguza vita kati ya Nchi mbalimbali, lakini vita katili za wenyewe kwa wenyewe zinaendelea kuwaua na kuwalemaza mamia ya maelfu ya watu kila mwaka.
Kwa nini? Kwa sababu bado kuna chuki kati ya vikundi vya kikabila, vya kijamii, na vya kidini—kisababishi cha vita za wenyewe kwa wenyewe. Na biashara mbalimbali ulimwenguni pote na magenge ya wahalifu huuza silaha nyingi za bei rahisi kwa vikundi vinavyopigana. Umoja wa kweli hauwezi kutokezwa na mashine za elektroniki. Wala ongezeko la faida katika soko la hisa haliwezi kutokeza haki katika jamii.
Katika njia fulani, utandaridhi wa kiuchumi unaweza kusababisha mgawanyiko. Uchumi unapoanza kuzorota baada ya kuimarika sana, wanasiasa wakatili wanaweza kutumia nafasi hiyo ili kujifaidi na kuwanyanyasa maskini wasio na uwezo. Basi suluhisho ni nini? Kichapo cha Human Development Report 1999 kinasema hivi: “Ni lazima kuwe na usimamizi mpya katika mataifa na ulimwenguni pote—na hangaiko kuu liwe kuleta usawa na kuwawezesha watu kufanya maendeleo.” Ufalme wa Mungu utafanya hivyo hasa.
-