-
Kwa Nini Yehova Alituumba?Jinsi ya Kupata Maisha Yenye Kuridhisha
-
-
Ugunduzi wa hivi karibuni kuhusu chembe za binadamu unaonyesha nini?
Wanasayansi wanaamini kwamba sasa wanafahamu jambo linalosababisha chembe zizeeke. Visehemu vya chembe za urithi vinavyoitwa telomere, vinavyopatikana kwenye miisho ya kromosomu, huwa fupi kila mara chembe inapogawanyika. Baada ya chembe kugawanyika mara 50 hadi 100, telomere huchakaa, na chembe nyingi huacha kugawanyika. Lakini ugunduzi wa hivi karibuni wa kisayansi unadokeza kwamba kwa msaada wa kimeng’enya kinachoitwa telomerase, chembe za binadamu zinaweza kuendelea kugawanyika milele.
-