Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuufanya Ulimwengu Uwe na Uraibu wa Dawa za Kulevya
    Amkeni!—1999 | Novemba 8
    • Jambo linalofanya hali iwe mbaya zaidi, ni kwamba katika miaka ya hivi majuzi, kumekuwako dawa za kulevyab za kubuniwa. Kemikali hizo za sanisia zimebuniwa kumfanya mtumiaji apumbae au ahisi furaha. Kwa kuwa dawa za kulevya za kubuniwa zinaweza kutengenezwa kwa bei rahisi karibu mahali popote, polisi hawana uwezo kabisa wa kuzidhibiti. Mnamo 1997, Tume ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulika na Dawa za Kulevya ilionya kwamba katika nchi nyingi dawa hizi za kubuniwa zimekuwa sehemu ya “utamaduni wa watumiaji wengi” na kwamba zapasa kuonwa kuwa “tisho kubwa kwa jumuiya ya kimataifa katika karne ijayo.”

      Dawa za kulevya mpya zaidi ni zenye matokeo sawa na zile zilizotangulia. Kokeini iliyosafishwa hutokeza uraibu hata zaidi ya kokeini ya kawaida. Aina mpya za bangic zinatokeza njozi nyingi zaidi, na dawa mpya ya kulevya ya kubuniwa inayoitwa ice huenda ikawa miongoni mwa dawa zenye madhara makubwa zaidi.

  • Kuufanya Ulimwengu Uwe na Uraibu wa Dawa za Kulevya
    Amkeni!—1999 | Novemba 8
    • b Dawa ya kulevya ambayo imefanyiwa marekebisho madogo katika muundo wake wa kemikali, mara nyingi hutokezwa ili kukwepa vizuizi vya dawa za kulevya haramu au dawa zenye kuleta njozi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki