-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Obadia, cha Yona, na cha MikaMnara wa Mlinzi—2007 | Novemba 1
-
-
Kwa sababu ya ibada yao ya sanamu, nchi za Israeli na Yuda zinastahili “upara,” au aibu. Kwa kupelekwa utekwani, upara wao ungepanuliwa “kama ule wa tai.” Inaelekea tai huyo ni aina fulani ya ndege anayewinda ambaye ana nywele chache laini kwenye kichwa chake.
-