Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Pia, dunia ipo umbali ufaao zaidi kutoka kwenye jua, jambo ambalo ni muhimu kwa uhai kusitawi. Mtaalamu wa nyota John Barrow na mtaalamu wa hesabu Frank Tipler walichunguza “ulinganisho wa nusu-kipenyo ya Dunia na umbali kutoka kwenye Jua.” Wao walikata kauli kwamba wanadamu hawangeweza kuishi “iwapo ulinganisho huo ungekuwa tofauti kidogo na jinsi ulivyo sasa.” Profesa David L. Block asema: “Hesabu inaonyesha kwamba kama dunia ingalikuwa karibu na jua kwa asilimia 5 tu, joto jingi kupita kiasi lingetukia miaka milioni 4 000 iliyopita. Ikiwa, kwa upande mwingine, dunia ingalikuwa mbali zaidi na jua kwa asilimia 1 tu, barafu nyingi zingalifunika dunia miaka ipatayo milioni 2 000 iliyopita.”—Our Universe: Accident or Design?

  • Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Jambo jingine dogo lililo muhimu ni njia ya dunia yetu kulizunguka jua. Nyota-mkia zina njia pana zenye umbo la yai. Kwa uzuri, sivyo ilivyo na dunia. Mzunguko wake ni karibu uwe duara kabisa. Tena hii inatuzuia tusipatwe na joto kali sana au baridi kali sana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki