-
Sakafu ya Bahari—Siri Zake ZafunuliwaAmkeni!—2000 | Novemba 22
-
-
TWAHITAJI kuelewa kindani kidogo jinsi ambavyo dunia imeumbwa ili tuweze kuelewa mambo yaliyoonwa na watafiti waliokuwa kwenye chombo cha Alvin. Yaaminika kuwa dunia yetu imefanyizwa na tabaka thabiti (linaloitwa lithosphere) linalokalia mwamba ulioyeyuka, unaosogea polepole. Kwa wazi, tabaka thabiti la nje lina kina cha takriban kilometa 100 nalo hufanyiza asilimia 0.6 hivi tu ya dunia yote. Tabaka la nje kabisa, si laini, ni nene mno chini ya mabara na jembamba kiasi cha kilometa sita chini ya safu ya milima iliyo katikati ya bahari.
Isitoshe, tabaka hilo thabiti la nje si zima kama ganda la yai, bali limegawanyika. Badala yake, laonekana likiwa limegawanyika katika mabamba kadhaa makubwa yaliyo thabiti, na mengine mengi madogo, yote huitwa miamba mikuu (tectonic plates). Miamba hiyo hufanyiza mabara na mabonde ya bahari. Miamba hiyo husogea-sogea. Mahali inapotengana, inaacha pengo na kutokeza nyufa katika safu ya milima ya katikati ya bahari. Ulimwenguni pote, miamba hiyo husogea kwa mwendo wa wastani wa sentimeta tatu hivi kwa mwaka.
-
-
Sakafu ya Bahari—Siri Zake ZafunuliwaAmkeni!—2000 | Novemba 22
-
-
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 4, 5]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Tabaka la juu la dunia
Tabaka la katikati (lililoyeyuka kwa kiasi fulani)
Bonde
Eneo la mshuko
Mwamba mkuu
Ufa
Miamba mikuu inapotengana, nyufa hutokea
[Picha]
Safu ya milima iliyo katikati ya bahari hujipinda-pinda kuzunguka dunia kama mshono ulio kwenye mpira wa tenisi
[Hisani]
NOAA/Department of Commerce
-