-
Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mimi nikaona kiti cha ufalme kikubwa cheupe na mmoja aliyeketi juu yacho. Kutoka mbele zake dunia na mbingu zikakimbilia mbali, na mahali hapakupatikana kwa ajili yazo.” (Ufunuo 20:11, NW)
-
-
Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
4. Maana yake nini kwamba “dunia na mbingu zikakimbilia mbali”?
4 Ni jinsi gani “dunia na mbingu zikakimbilia mbali”? Hii ni mbingu ile ile ambayo iliondoka kama hati-kunjo wakati wa kufunguliwa kifungo cha sita—serikali za kibinadamu zenye kutawala ambazo “zimewekwa akiba kwa ajili ya moto na zinawekwa kwa ajili ya siku ya hukumu na ya kuharibiwa kwa watu wasiohofu Mungu.” (Ufunuo 6:14; 2 Petro 3:7, NW) Dunia ni mfumo wa mambo uliopangwa kitengenezo ulio chini ya utawala huu. (Ufunuo 8:7) Uharibifu wa hayawani-mwitu na wafalme wa dunia na majeshi yao, pamoja na wale waliopokea alama ya hayawani-mwitu na wale waliotoa ibada kwa mfano wake, hutia alama ya kukimbilia mbali kwa hii mbingu na dunia. (Ufunuo 19:19-21)
-