Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Lakini mataifa yakawa yenye kujaa hasira-kisasi, na hasira-kisasi yako ikaja, na wakati uliowekwa rasmi kwa ajili ya wafu kuhukumiwa, na wa kuwapa thawabu zao watumwa wako manabii na watakatifu na wale wanaohofu jina lako, wadogo na wakubwa, na kuleta kwenye angamizo wale wanaoangamiza dunia.” (Ufunuo 11:18, NW) Kuanzia 1914 na kuendelea mataifa ya ulimwengu yameonyeshana hasira-kisasi kwa ukali, na dhidi ya Ufalme wa Mungu, na hasa dhidi ya mashahidi wawili wa Yehova.—Ufunuo 11:13.

      9. Mataifa yamekuwa yakiangamizaje dunia, naye Mungu ameazimu kufanya nini juu ya hilo?

      9 Katika muda wote wa historia mataifa yamekuwa yakiangamiza dunia kwa vita vyao visivyokoma na kwa usimamizi mbaya. Hata hivyo, tangu 1914 angamizo hili limechapua mwendo kwa kiwango chenye kuhofisha. Pupa na ufisadi vimetokeza kuenea kwa majangwa na kupotezwa sana kwa bara lenye kuzaa. Mvua ya asidi na mawingu ya redioaktivu vimeharibu maeneo makubwa. Vyanzo vya chakula vimechafuliwa. Hewa tunayopumua na maji tunayokunywa yametiwa uchafu. Takataka za viwandani hutisha kumaliza uhai katika bara na bahari. Na wakati fulani, mataifa yenye nguvu zaidi yalitisha kuleta angamizo kamili kwa njia ya kufutilia mbali kabisa aina yote ya kibinadamu kwa vita ya nyukilia.

  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 175]

      Kuangamiza Dunia

      “Kila nukta tatu kisehemu cha msitu asili wenye kuleta mvua ukubwa wa kiwanja cha mpira hutoweka. . . . Upotevu wa msitu asilia unaharibu maelfu ya aina za mimea na za wanyama.”—Illustrated Atlas of the World (Rand McNally).

      “Katika karne mbili za ukazi, [Maziwa Makubwa] yamekuwa pia dimbwi la takataka la ulimwengu lililo kubwa zaidi ya yote.”—The Globe and Mail (Kanada).

      “Katika Aprili 1986 mlipuko na moto kwenye kiwanda cha nguvu za nyukilia katika Chernobyl, Urusi, “ulikuwa ndio tukio la nyukilia lenye maana zaidi sana . . . tangu kubomiwa kwa Hiroshima na Nagasaki,” likitokeza “mnururisho mwingi wa muda mrefu katika hewa, udongo-juu na maji ya ulimwengu kama majaribio yote ya nyukilia na mabomu yaliyopata kulipuliwa.”—JAMA; The New York Times.

      Katika Minamata, Japani, kiwanda cha kemikali kilidondosha kemikali ya methilmekyuri ndani ya ghuba. Kula samaki na samakimagamba waliochafuliwa na mdondosho huo kulitokeza ugonjwa wa Minamata (UM) “ugonjwa wa neva wenye kusedeka. . . . Leo hii [1985], imehakikishwa rasmi kuwa watu 2578 kotekote Japani wana UM.”—International Journal of Epidemiology.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki