-
Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
-
-
Gazeti Healthy Eating hutoa sababu hii juu ya kwa nini huenda tusijali kwa habari ya mazoea yetu ya ulaji, ingawa twajua kwamba ulaji mzuri ni muhimu kwa uhai: “Tatizo ni kwamba [likiwa tokeo la mazoea mabaya ya ulaji] afya hudhoofika polepole, hakuna tokeo la ghafula kama lile ambalo hufuata uvukaji barabara ovyoovyo. Badala ya hivyo, huenda afya ya mtu ikadhoofika polepole sana bila kujulikana, huenda akaambukizwa kwa urahisi, huenda mifupa ikawa dhaifu zaidi, kupona kwa majeraha na maradhi huenda kukawa kwa polepole zaidi.”
-
-
Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
-
-
Katika visa vyenye kupita kiasi mtu huenda akawa kama mwanamke kijana anayepatwa na hali ya kuhofu sana kunenepa. Yeye hujisadikisha kwamba hahitaji chakula kingi, kwamba yeye ni mzima kabisa, ijapokuwa jambo la kwamba yeye anadhoofika kimwili. Mwishowe yeye hupoteza hamu yote ya kula. “Ni hali hatari,” chasema kitabu kimoja cha marejezo. Kwa nini? “Ijapokuwa ni mara chache mgonjwa hufa njaa kihalisi, yeye huwa amekosa kabisa lishe bora na huenda akashindwa na maambukizo ambayo kwa kawaida yangekuwa madogo-madogo.”
-