Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/12 uku. 7
  • Uwe na Lengo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uwe na Lengo
  • Amkeni!—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Unaweza Kutimiza Malengo Yako ya Kiroho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Je, Niache Shule?
    Amkeni!—2010
  • Niyatumieje Maisha Yangu?
    Amkeni!—2006
  • Je, Niache Shule?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 10/12 uku. 7

Uwe na Lengo

[Picha katika ukurasa wa 7]

Shule inakuwa na maana zaidi—na inafurahisha zaidi—unapojua elimu inakufaidi kwa njia gani.

KWENDA shule bila kuwa na lengo lolote ni kama kukimbia mbio zisizo na mwisho. Biblia inasema hivi: “Jua unakoelekea.” (Methali 4:26, Contemporary English Version) Kuwa na lengo kutakufanya ukazie fikira jambo hususa na kutarahisisha mambo utakapoanza kufanya kazi. Unawezaje kujiwekea lengo?

Jiulize, ‘Ninapanga kujiruzuku kwa njia gani?’ Usiahirishe kujibu swali hilo. Badala yake, anza kufanya mipango mapema. Kwa nini? Linganisha jambo hilo na mfano huu: Ukitaka kwenda safari, kwanza lazima uamue unataka kwenda wapi. Kisha ukitumia ramani, utaamua ni njia ipi itakayokusaidia kufika huko kwa urahisi. Unaweza kutumia mbinu hiyo kuhusu elimu yako. Fikiria kazi unayotaka kufanya, na kisha uchague masomo yatakayokusaidia kufika unakoelekea.

Tahadhari: Vijana wengi wanataka kufanya kazi wanazopenda tu​—kwa mfano wanataka kuwa wanamuziki maarufu—​hivi kwamba hawataki kufikiria kufanya kazi nyingine. Ni njia gani bora zaidi ya kuchagua kazi?

  1. Fikiria uwezo wako. Kwa mfano, je, wewe hufurahia kazi za kuwahudumia wengine? Je, wewe ni stadi katika umekanika? hesabu? uhasibu? au kurekebisha vitu?

  2. Chunguza kazi ulizochagua. Ni kazi gani zinazopatana zaidi na uwezo wako? Badala ya kukazia fikira kazi moja tu ambayo unaiona kuwa ndiyo “inayofaa zaidi,” zungumzia kazi nyingine zinazofaa pamoja na watu wengine. Na uone mambo kihalisi. Kwa mfano, je, kazi unayotaka inaweza kupatikana katika maeneo mengine, ikiwa wakati mmoja utahama? Je, masomo unayohitaji kwa ajili ya kazi hiyo yatakuingiza katika deni kubwa?

  3. Chunguza nafasi zilizopo. Baada ya kuamua ni kazi gani ungependa kufanya, chunguza ikiwa kuna nafasi za kuajiriwa katika eneo unamoishi. Unajua watu wowote wanaoweza kukuajiri? Ikiwa ndivyo, je, wao humwajiri mtu wakiwa na lengo la kumfunza mtu kazi hiyo? Je, kuna programu za kupata mazoezi ya kiufundi?

Dokezo: Waulize wazazi, walimu, na watu wazima walio marafiki wako. Chunguza nafasi za kazi zilizoorodheshwa kwenye magazeti au sehemu nyingine.

Jambo kuu: Ukiwa na lengo, elimu yako itakuwa na mwelekeo na kusudi.

Anza sasa! Ukiwa bado shuleni, fikiria kuhusu mambo matatu yaliyozungumziwa hapo juu. Andika malengo yako, na uyazungumzie pamoja na wazazi wako.

Huenda umeona kwamba mfululizo huu ulitaja Biblia mara nyingi ulipozungumzia njia za kufanikiwa shuleni. Mashahidi wa Yehova ambao ndio huchapisha gazeti hili, wanaamini kwamba “Maandiko yanatuelimisha sisi katika mambo yote.” (2 Timotheo 3:16, Biblia ya Kiswahili, maelezo ya chini) Biblia ina mashauri kwa ajili ya maisha ya kila siku​—si shuleni tu, bali pia kazini, katika familia, na sehemu nyingine za maisha.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki