-
Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 15
-
-
Watu fulani wanadhani kwamba desturi hiyo ilianza wakati miili ilipopatikana ikiwa imehifadhiwa ndani ya magadi, ambayo ni aina ya chumvi inayopatikana kwa wingi nchini Misri na maeneo yanayoizunguka.
-
-
Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 15
-
-
Wamisri wa kale walihifadhi wafu hasa kwa sababu za kidini. Dhana yao ya uhai baada ya kifo ilihusiana na tamaa ya wafu kuendelea kuwasiliana na walio hai. Waliamini kwamba miili yao ingeendelea kutumiwa kwa umilele na kwamba ingerudishiwa uhai tena. Ijapokuwa desturi ya kuhifadhi maiti ilikuwa ya kawaida, kufikia sasa hakuna habari yoyote ambayo imepatikana kuhusu jinsi Wamisri walivyohifadhi maiti. Habari iliyo bora inayopatikana ni ile ya Herodoto, mwanahistoria Mgiriki wa karne ya tano K.W.K. Hata hivyo, imeripotiwa kwamba kujaribu kuhifadhi maiti kwa kufuata mielekezo iliyotolewa na Herodoto hakujafanikiwa sana.
-
-
Je, Inafaa Wakristo Kuhifadhi maiti kwa Kuipaka Dawa?Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 15
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 31]
KUPAKA MAITI DAWA—WAKATI ULIOPITA NA SASA
Katika Misri ya kale njia ambayo ilitumiwa kupaka maiti dawa ili isioze ilitegemea hali ya familia. Yaelekea familia yenye utajiri ingefuata utaratibu huu:
Ubongo ungetolewa kwenye fuvu kupitia mianzi ya pua kwa kutumia kifaa cha chuma. Baada ya hilo, fuvu lingepakwa dawa. Jambo lililofuata lilitia ndani kuondoa viungo vyote vilivyo ndani ya mwili isipokuwa moyo na figo. Kufikia viungo vilivyo ndani ya tumbo, mwili ulihitaji kupasuliwa, lakini jambo hilo lilionwa kuwa dhambi. Ili kuepuka jambo hilo lenye ubishi, Wamisri waliopaka maiti dawa walimchagua mtu waliyemwita mkataji ili kufanya upasuaji huo. Mara tu alipopasua maiti, alitoroka ili kuepuka kuadhibiwa kwa kulaaniwa na kupigwa kwa mawe kwa sababu ya upasuaji huo ulioitwa eti uhalifu.
Baada ya matumbo kuondolewa, tumbo lilioshwa kabisa. Mwanahistoria Herodoto aliandika: “Walijaza tumbo kwa vipande vya manemane safi pamoja na mdalasini na viungo vya aina nyingine mbalimbali isipokuwa uvumba, kisha walishona mahali palipopasuliwa.”
Baadaye, mwili ulikaushwa kwa kuwekwa ndani ya magadi kwa siku 70. Kisha maiti hiyo ilioshwa kwa ustadi na kufungwa kwa kitani. Halafu kitani hicho kilifunikwa kwa utomvu wa aina fulani uliotumika kama gundi, kisha mummy (maiti iliyopakwa dawa) iliwekwa kwenye sanduku la mbao lililorembwa sana na lililokuwa na umbo la binadamu.
-