Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dumisha Amani Nyumbani Mwako
    Siri ya Furaha ya Familia
    • 20. Huenda watoto wakawa na hisia gani ikiwa baba au mama yao ni mzazi wa kambo?

      20 Katika nyumba nyingi hali inayotokeza ugumu mkubwa zaidi si ya kidini bali ni ya kiuzazi. Nyumba nyingi leo hutia ndani watoto kutoka ndoa za awali za mzazi mmoja au wote wawili. Katika familia ya jinsi hiyo, huenda watoto wakawa na hali ya wivu na uchungu au labda kupingana kwa uaminifu-mshikamanifu. Likiwa tokeo, huenda wakapinga jitihada zenye moyo mweupe za mzazi huyo wa kambo za kuwa baba au mama mwema. Ni nini kiwezacho kusaidia kufanya familia ya kambo iwe yenye mafanikio?

  • Dumisha Amani Nyumbani Mwako
    Siri ya Furaha ya Familia
    • 22. Kwa nini huenda watoto wakaliona kuwa jambo gumu kumkubali mzazi wa kambo?

      22 Ikiwa wewe ni mzazi wa kambo, huenda ukakumbuka kwamba ukiwa rafiki ya hiyo familia, labda ulikaribishwa na watoto. Lakini ulipogeuka kuwa mzazi wao wa kambo, huenda ikawa mtazamo wao ulibadilika. Wakimkumbuka mzazi wao halisi ambaye haishi nao tena, huenda watoto wakawa wanang’ang’ana na kupingana kwa uaminifu-mshikamanifu, labda wakihisi kwamba wewe wataka kuondolea mbali shauku waliyo nayo kuelekea mzazi ambaye hayupo. Nyakati nyingine, huenda wakakukumbusha kwa njia isiyo ya adabu kwamba wewe si baba yao au si mama yao. Maneno hayo yanaumiza. Hata hivyo, “usifanye haraka kukasirika [“kuwa mwenye kuudhika,” NW] rohoni mwako.” (Mhubiri 7:9) Ufahamu na hisia-mwenzi zahitajiwa ili kushughulikia hisia-moyo za watoto.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki