Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Harara ya kizalendo imechochewa, nalo dhehebu la ibada ya maliki lina kifano cha ki-siku-hizi kwa namna ya wimbi la utukuzo wa taifa ambao umeenea pote duniani.

  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika United States, mamia ya watoto na walimu walifukuzwa shuleni kwa sababu hawakusalimu bendera ya kitaifa, hali katika Ujeremani Mashahidi walinyanyaswa vikali kwa kukataa kusalimu swastika. Kama ilivyokwisha kuonyeshwa, Wanazi wa Hitla waliua watumishi washikamanifu wa Yehova kwa sababu walikataa kushiriki ibada ya sanamu kama hiyo ya kitaifa. Katika miaka ya 1930, wakati wa usitawi mwingi wa ibada ya Shinto ya maliki wa Japani, wahudumu wawili mapainia walipanda mbegu nyingi za Ufalme katika Taiwani iliyokaliwa na Wajapani. Watawala wa kivita waliwatupa gerezani, ambamo mmoja wao alikufa kwa sababu ya kutendwa kikatili. Yule mwingine aliachiliwa baadaye, akaja tu kupigwa risasi mgongoni—Antipasi wa ki-siku-hizi. Mpaka leo hii, kuna mabara ambamo ibada ya mifano ya kitaifa na kujitoa kabisa kabisa kwenye serikali ni mambo yanayodaiwa. Mashahidi wengi vijana wametiwa gerezani, na si wachache wakafishwa, kwa sababu ya msimamo wao wa ushujaa wakiwa Wakristo wasiokuwamo.

  • Kushikilia kwa Imara Jina la Yesu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 7. Vijana wachanga katika India walikabilije suala la ibada ya utukuzo wa taifa, na kwa tokeo gani?

      7 Walio wachanga wameelekeana na masuala kama hayo shuleni. Katika 1985 katika mkoa wa Kerala, India, watoto watatu wachanga wa Mashahidi wa Yehova walikataa kuacha msimamo wao uliotegemea imani ya Biblia, wakikataa kuimba wimbo wa kutukuza taifa. Wao walisimama kwa heshima huku wengine wakiimba, lakini hata hivyo walifukuzwa shuleni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki