-
Nitapata Pesa Wapi?Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
-
-
Tayarisha na usambaze nakala za tawasifu yako. Andika kwenye karatasi jinsi unavyoweza kupatikana na kuorodhesha ujuzi na uzoefu wa kazi ulio nao. Huenda ukadhani kwamba huna chochote cha kuandika. Umekosea. Je, umewahi kumtunza mdogo wako wakati ambapo wazazi wako hawakuwako, au kumtunzia mtu mwingine watoto? Hilo linaonyesha kwamba unategemeka. Umewahi kumsaidia baba yako kurekebisha gari? Huenda hilo likaonyesha kwamba una akili ya kurekebisha vitu. Je, unajua kupiga chapa au kutumia kompyuta? Au je, ulipata alama za juu shuleni katika mradi fulani? Hayo ni mambo mazuri yanayoweza kuwavutia waajiri fulani. Yaorodheshe katika tawasifu yako. Wape waajiri mbalimbali tawasifu yako na kuwaomba marafiki na watu wa ukoo wampe mtu yeyote anayetafuta wafanyakazi.
-
-
Nitapata Pesa Wapi?Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
-
-
PENDEKEZO
Tuma vyeti vyako kwa kampuni mbalimbali badala ya kungoja watangaze nafasi za kazi zilizopo.
-