Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mbinu Tano za Kutafuta Kazi
    Amkeni!—2005 | Julai 8
    • Toa Habari Kamili Kuhusu Elimu na Ujuzi

      Wale wanaotoa maombi ya kazi za usimamizi, lazima waandike na kusambaza habari kuhusu elimu na ujuzi wao. Lakini hata iwe unatafuta kazi gani, habari kamili kuhusu elimu na ujuzi ulio nao inaweza kusaidia sana. Nigel, mshauri wa kazi huko Australia, anasema: “Habari kuhusu elimu na ujuzi wako huwafahamisha waajiri juu yako na mambo ambayo umetimiza na kwa nini wanakuhitaji.”

      Utaandika habari gani? Andika jina lako kamili, anwani, namba ya simu, na anwani ya barua-pepe. Taja lengo lako. Taja elimu uliyo nayo na pia mazoezi na stadi ambazo umepata zinazohusiana na kazi unayotafuta. Toa habari kamili kuhusu kazi ambazo umefanya hapo awali. Taja ulichofanya na pia miradi uliyofikia na manufaa uliyoletea kampuni uliyokuwa ukifanyia kazi. Pia taja mambo uliyofanya katika kazi yako ya awali ambayo yanafanya ustahili kazi unayotafuta. Tia ndani habari za kibinafsi zinazofafanua sifa na mapendezi yako. Kwa kuwa mahitaji ya kampuni hutofautiana, huenda ukahitaji kubadili habari unazotoa kila unapotoa maombi ya kazi.

      Je, unapaswa kutoa habari kuhusu elimu na ujuzi wako ikiwa unatafuta kazi kwa mara ya kwanza? Ndiyo! Huenda umefanya mambo mengi yanayoweza kuonwa kuwa ujuzi wa kazi. Kwa mfano, je, unapenda useremala au labda kurekebisha magari makuukuu? Unaweza kutaja mambo hayo. Je, umewahi kufanya kazi yoyote ya kujitolea? Taja kazi ya kujitolea ambayo umewahi kufanya na miradi uliyofikia.—Ona sanduku “Sampuli ya Habari Kuhusu Elimu na Ujuzi kwa Wasio na Ujuzi wa Kazi.”

      Usipopata nafasi ya kumwona mtu unayetazamia akuajiri, acha kadi ndogo, ikiwezekana yenye ukubwa wa sentimeta 10 kwa sentimeta 15, ambayo ina jina, anwani, namba ya simu, na anwani ya barua-pepe, kutia ndani maelezo mafupi kuhusu ustadi wako na mambo ambayo umetimiza. Ikifaa, unaweza kubandika picha yako nyuma ya kadi hiyo. Wape kadi hiyo watu ambao wanaweza kukusaidia kupata kazi na uwaombe wampe mtu yeyote wanayemjua ambaye ana kazi unayotafuta. Mwajiri akiona kadi hiyo, anaweza kukupa nafasi ya mahojiano, au labda akuajiri!

      Kuandika habari kuhusu elimu na ujuzi wako kunaweza kufanya uhisi ukiwa na uhakika unapotafuta kazi. Nigel, aliyetajwa hapo awali anasema: “Kuandika habari kuhusu elimu na ujuzi wako kunaweza kukusaidia upange mawazo na miradi yako. Pia kunafanya uwe na uhakika kwa sababu kutakusaidia ujitayarishe kwa ajili ya maswali ambayo huenda ukaulizwa wakati wa mahojiano ya kazi.”—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 7.

  • Mbinu Tano za Kutafuta Kazi
    Amkeni!—2005 | Julai 8
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 6]

      Sampuli ya Habari Kuhusu Elimu na Ujuzi kwa Wasio na Ujuzi wa Kazi

      Jina Lako:

      Anwani Yako:

      Namba Yako ya Simu na Anwani ya Barua-pepe:

      Tarehe ya Kuzaliwa:

      Lengo: Kutafuta kazi yoyote katika kiwanda.

      Elimu: Nilihitimu Shule ya Upili ya Kwetu katika mwaka wa 2004.

      Masomo: Lugha za kigeni, hisabati, kompyuta, useremala.

      Ustadi na Uwezo: Mimi hufanya kazi za mikono kwa ustadi. Hurekebisha gari la familia kwa ukawaida. Nilitengeneza viti na meza ya mbao nyumbani. Hufurahia kutumia ustadi wangu wa hisabati ninapotengeneza vitu vya mbao. Niliezeka paa katika mradi wa ujenzi wa kujitolea. Ninaweza kutumia kompyuta mbalimbali nami hufurahia kujifunza programu mpya za kompyuta.

      Habari za Kibinafsi: Ninategemeka—nilikosa kwenda shule siku mbili tu nilipokuwa kidato cha mwisho. Mimi ni mnyoofu—nilirudisha kibeti chenye pesa kilichokuwa kimepotea. Mimi ni mwenye urafiki—ninafanya kazi ya kujitolea katika jamii kwa ukawaida, nami hufurahia kuwasaidia wazee. Michezo—ninapenda kucheza mpira wa vikapu. Ninapenda useremala na kurekebisha magari.

      Watu Wanaonipendekeza: Majina yao yatapatikana yakiombwa.a

      [Maelezo ya Chini]

      a Watu watakaokupendekeza wanaweza kutia ndani mwalimu anayekujua vizuri au mfanyabiashara ambaye ni rafiki wa familia. Mwajiri akiomba majina hayo, hiyo ni ishara ya mapema kwamba huenda akataka kukuajiri. Hakikisha kwamba umewaomba ruhusa wale unaotaka wakupendekeze.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki