-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Wazazi wa Esta walipokufa, mmoja wa watu wake wa ukoo, mwanamume mwenye huruma anayeitwa Mordekai, alimsikitikia mtoto huyo. Mordekai alikuwa binamu ya Esta, lakini alikuwa na umri mkubwa zaidi. Alimchukua Esta na kumlea kama binti yake.—Esta 2:5-7, 15.
Mordekai na Esta walikuwa Wayahudi waliohamishwa na waliishi katika mji mkuu wa Waajemi, ambako huenda walidhihakiwa kwa sababu ya dini yao na Sheria ambazo walijitahidi kufuata. Lakini ni wazi kwamba Esta alisitawisha uhusiano wa karibu na binamu yake alipokuwa akimfundisha kuhusu Yehova, Mungu mwenye rehema ambaye aliwaokoa watu wake hapo zamani kutoka katika matatizo mengi—na ambaye angewaokoa tena. (Mambo ya Walawi 26:44, 45) Kwa kweli, uhusiano wa karibu na wenye upendo uliimarika kati ya Esta na Mordekai.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Watumishi wa mfalme walimwona Esta na kumchukua kutoka kwa Mordekai, kisha wakampeleka kwa jumba la kifahari la mfalme lililokuwa ng’ambo ya mto. (Esta 2:8) Kwa kweli, haikuwa rahisi kwa Esta na binamu yake kuachana, kwa sababu walikuwa kama baba na binti yake. Mordekai hakutaka Esta aolewe na mtu asiyeamini Mungu, hata awe mfalme, lakini hangeweza kuzuia jambo hilo. Kabla hajachukuliwa, lazima Esta awe alisikiliza kwa makini mashauri ya Mordekai.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Bila shaka, Mordekai alijali sana hali ya Esta. Tunasoma kwamba siku baada ya siku, alienda karibu wa nyumba ya wanawake ili apate kujua hali ya Esta. (Esta 2:11) Habari chache alizopata, labda kutoka kwa wafanyakazi walioshirikiana naye, lazima zilimfurahisha sana.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Kwa mfano, tunasoma: “Esta hakuwa amesema kuhusu watu wake wala kuhusu jamaa zake, kwa maana Mordekai alikuwa amemwamuru kwamba asiseme.” (Esta 2:10) Mordekai alikuwa amemwagiza msichana huyo asifunue kwamba yeye ni Myahudi; bila shaka Mordekai alijua kuwa mamlaka ya Waajemi iliwabagua watu wake. Lilikuwa jambo lenye kupendeza kama nini kwa Mordekai kujua kwamba ingawa Esta hukuwa karibu naye, bado aliendelea kuwa mwenye hekima na mtiifu!
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Bila shaka, hapana! Esta aliendelea kumheshimu Mordekai, baba yake mlezi. Hakufunua kwamba yeye ni Myahudi. Zaidi ya hayo, Mordekai alipomweleza kuhusu njama ya kumuua Ahasuero, kwa utii Esta alimweleza mfalme, na watu waliopanga njama hiyo wakauawa. (Esta 2:20-23)
-