-
Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu WetuMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Ingawa tayari kulikuwa kumekuwa mikusanyiko mingi ya kimataifa, lililotukia katika 1963 lilikuwa la kwanza la aina yake. Ulikuwa mkusanyiko wa ulimwenguni pote. Ukianzia Milwaukee, Wisconsin, katika Marekani, ulisonga mbele kwenda New York; kisha, kwenye majiji makubwa manne katika Ulaya; kupitia Mashariki ya Kati; kusonga mbele hadi India, Burma (sasa Myanmar), Thailand, Hong Kong, Singapore, Filipino, Indonesia, Australia, Taiwan, Japani, New Zealand, Fiji, Jamhuri ya Korea, na Hawaii; na kisha kurudi kwenye bara la Amerika Kaskazini. Kwa ujumla, wajumbe kutoka nchi 161 walikuwapo. Jumla ya hudhurio ilizidi 580,000. Walikuwapo 583, kutoka nchi kama 20, walioandamana na mkusanyiko, wakihudhuria katika nchi moja baada ya nyingine, duniani pote. Safari za utalii za pekee ziliwawezesha kuona sehemu za kidini zenye kupendeza, na pia walishiriki pamoja na ndugu na dada wenyeji katika huduma ya nyumba hadi nyumba. Wasafiri hao walijilipia gharama zao wenyewe.
-
-
Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu WetuMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 277]
Katika 1963 mkusanyiko wa ulimwenguni pote ulifanywa, wajumbe kutoka nchi zipatao 20 wakisafiri nao duniani pote
Kyoto, Japani, (chini kushoto), lilikuwa moja la majiji 27 ya mkusanyiko. Wajumbe katika Jamhuri ya Korea walipata kujuana (katikati). Salamu ya Kimaori katika New Zealand (chini kulia)
-