-
Mageuzi—Dhana na Ukweli wa MamboUhai—Ulitokana na Muumba?
-
-
Broshua iliyochapishwa mnamo 1999 na Shirika la Kitaifa la Sayansi (NAS) nchini Marekani ilirejelea “spishi 13 za shore waliochunguzwa na Darwin katika Visiwa vya Galápagos, ambao leo wanaitwa shore wa Darwin.”23
Katika miaka ya 1970, watafiti kadhaa wakiongozwa na Peter R. na B. Rosemary Grant wa Chuo Kikuu cha Princeton, walianza kuwachunguza shore hao nao wakagundua kwamba baada ya mwaka mzima wa ukame katika visiwa hivyo, kulikuwa na shore wengi zaidi wenye midomo mirefu kuliko wale wenye midomo mifupi. Kwa kuwa mojawapo ya njia za msingi za kuainisha spishi 13 za shore ni kuchunguza ukubwa na umbo la midomo yao, matokeo ya uchunguzi huo yalionwa kuwa muhimu sana. Broshua hiyo ya NAS yaendelea kusema: “Akina Grant wamekadiria kwamba ukame ukitokea mara moja kila baada ya miaka 10 katika visiwa hivyo, baada ya miaka 200 hivi tu, spishi mpya ya shore itatokea.”24
Hata hivyo, broshua hiyo ya NAS inakosa kutaja kwamba katika miaka iliyofuata miaka ya ukame, kulikuwa na shore wengi zaidi wenye midomo mifupi. Watafiti hao waligundua kwamba jinsi hali ya hewa ilivyokuwa ikibadilika kisiwani, mwaka mmoja kulikuwa na shore wengi zaidi wenye midomo mirefu, lakini baadaye kukawa na shore wengi zaidi wenye midomo mifupi. Pia waligundua kwamba baadhi ya “spishi” hizo tofauti za shore zilizalishana kwa mtambuka na kutokeza vizazi vilivyostahimili vizuri zaidi kuliko vizazi vya awali. Walikata kauli kwamba ikiwa ndege hao wangeendelea kuzalishana kwa njia hiyo, “spishi” hizo mbili hatimaye zingeungana na kuwa spishi moja.25
Shore wa Darwin wanathibitisha jambo moja tu, kwamba wanaweza kuzoeleana na mazingira mageni
-
-
Mageuzi—Dhana na Ukweli wa MamboUhai—Ulitokana na Muumba?
-
-
Kwa kweli, shore wa Darwin hawajabadilika na kuwa “kitu chochote kipya.” Bado wao ni shore. Na uhakika wa kwamba shore hao wanazalishana kwa mtambuka unafanya mbinu za wanamageuzi fulani za kuainisha spishi zitiliwe shaka. Isitoshe, utafiti kuhusu ndege hao umefichua kwamba hata taasisi za kisayansi zenye kuheshimika zinaweza kuripoti matokeo ya utafiti mbalimbali zikiegemea upande mmoja.
-