-
Je, Kumwamini Mungu Ni Jambo Lisilopatana na Sayansi?Amkeni!—2004 | Juni 22
-
-
Wanasayansi wengi hukubali waziwazi kwamba wanaamini kuwapo kwa Muumba. Ni kweli kwamba huenda wasiamini kwamba kuna Mungu mwenye utu au huenda wasiiamini Biblia. Hata hivyo, wanasadiki kwamba ubuni uliopo ulitokana na Mbuni mwenye akili.
Je, wanasayansi hao wanaweza kuitwa washamba? Ikieleza kuhusu wanasayansi wanaoamini kwamba ulimwengu wetu na viumbe vilivyopo vilibuniwa kwa akili, makala moja katika gazeti The New York Times inasema hivi: “Wana shahada za juu zaidi na vyeo maarufu katika baadhi ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa sana. Dhana zao zinazopinga nadharia ya Darwin hazitegemei Maandiko; badala yake zinategemea kanuni za sayansi.”
Makala hiyohiyo pia inataja kwamba wale wanaounga mkono dhana ya kwamba ulimwengu umebuniwa kwa akili “hawatoi madai ya kipuuzi. . . . Wanachopinga ni kwamba nadharia ya Darwin, au nadharia nyingine yoyote inayodai kwamba uhai ulitokea wenyewe hatua kwa hatua inatosha kueleza chanzo cha uhai. Wanadai kuwa vitu vyenye uhai vinathibitisha wazi kwamba vimebuniwa kwa ustadi, jambo linalothibitisha kwa kadiri kubwa kuwapo kwa Mbuni Mwenye Akili.”a
Inashangaza kwamba kuna wanasayansi wengi wanaoamini hivyo. Kwa mfano, matokeo ya uchunguzi yaliyotolewa mwaka wa 1997 yalionyesha kwamba asilimia 40 ya wanasayansi wa Marekani wanaamini kuna Mungu mwenye utu. Idadi hiyo haikuwa imebadilika tangu mwaka wa 1914, wakati ambapo uchunguzi kama huo ulifanywa.
Katika nchi zisizo na wafuasi wengi wa dini kama vile nchi za Ulaya, idadi hiyo ni ndogo kwa kulinganishwa. Hata hivyo, gazeti la Uingereza, The Guardian liliripoti kwamba “wataalamu wa sayansi ngumu, kama vile fizikia na jiolojia, wanaoamini kuwapo kwa Mungu ni wengi kuliko wataalamu wa sayansi rahisi kama vile anthropolojia.” Gazeti hilo liliongezea hivi: “Huko Uingereza kuna mashirika kama vile shirika la Wakristo Katika Ulimwengu wa Sayansi.” Gazeti hilo lilisema pia kwamba huko Uingereza “idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wa sayansi huenda kanisani kuliko idadi ya wanafunzi wa sanaa.”
Hata hivyo, inaonekana kwamba wanasayansi wengi hudharau maoni ya kwamba kuna Muumba. Maoni yao yanawaathiri sana wanasayansi wenzao. Mtaalamu wa anga Allan Sandage anasema kwamba “mtu husita kujitambulisha kuwa muumini.” Kwa nini? Anasema kwamba “kuna shutuma kali na dhihaka nyingi kutoka kwa wanasayansi wengine.”
Kwa hiyo, wanasayansi wanaojaribu kudokeza kwamba sayansi haipingi kuwapo kwa Muumba, huzimwa na wale wanaotilia shaka jambo hilo.
-
-
Je, Kumwamini Mungu Ni Jambo Lisilopatana na Sayansi?Amkeni!—2004 | Juni 22
-
-
a Wasomi na wanasayansi maarufu ambao wameunga mkono hadharani wazo la kuwapo kwa Mbuni Mwenye Akili ni pamoja na Phillip E. Johnson, mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha California huko Berkeley; mtaalamu wa biokemia Michael J. Behe, mwandishi wa kitabu Darwin’s Black Box—The Biochemical Challenge to Evolution; mwanahisabati William A. Dembski; mwanafalsafa wa mantiki Alvin Plantinga; wanafizikia John Polkinghorne na Freeman Dyson; mtaalamu wa anga Allan Sandage; na wengine wengi.
-
-
Kwa Nini Wanasayansi Fulani Humwamini Mungu?Amkeni!—2004 | Juni 22
-
-
Watu wengi wanaotumia akili wanaamini kwamba vipimo sahihi vilivyopo ulimwenguni havikutokea tu. John Polkinghorne, aliyekuwa mtaalamu wa fizikia kwenye Chuo Kikuu cha Cambridge, alisema: “Unapotambua kwamba sheria za kiasili zimewekwa kwa usahihi kabisa ili kufanyiza ulimwengu unaoonekana, jambo hilo linakufanya uanze kuamini kwamba ulimwengu haukutokea wenyewe tu, bali ulitokezwa kwa kusudi fulani.”
Mwanafizikia Mwaustralia Paul Davies alikuwa na maoni kama hayo. Anaandika hivi: “Ni wazi kwamba wanasayansi wengi . . . wanadhihaki wazo la kwamba huenda kuna Mungu au hata chanzo fulani kisicho na utu. Mimi sikubaliani nao. . . . Siwezi kuamini kwamba kuwa kwetu ulimwenguni kulitokea tu bila mpango, . . . kupitia tukio kubwa la kiholela lililofanyiza ulimwengu.”
-
-
Kwa Nini Wanasayansi Fulani Humwamini Mungu?Amkeni!—2004 | Juni 22
-
-
Kwa mfano, mwanahisabati William A. Dembski aliandika kwamba “vitu vilivyobuniwa kwa akili” vilivyo katika “ulimwengu unaoonekana . . . vinaweza tu kuwa vilitokana na mtu mwenye akili.” Mtaalamu wa biokemia ya molekuli Michael Behe anakata maneno kwa kusema hivi: “Unaweza kuwa Mkatoliki kwa dhati na bado uamini nadharia ya Darwin. Hata hivyo, biokemia imefanya iwe vigumu zaidi kuwa mwanasayansi mwenye kutumia akili na wakati uleule kuamini nadharia hiyo.”
-