-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha KutokaMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
‘MUNGU ALISIKIA KUUGUA KWAO’
Wazao wa Yakobo wanaoishi Misri wanaongezeka haraka sana hivi kwamba kwa amri ya mfalme wanateswa kwa kufanywa kuwa watumwa. Farao hata anatoa amri watoto wote wa kiume wa Israeli wauawe. Musa, mtoto mwenye umri wa miezi mitatu ambaye anachukuliwa na binti ya Farao awe mtoto wake, anaokoka mauaji hayo. Ingawa Musa analelewa katika nyumba ya mfalme, anapokuwa na umri wa miaka 40 anawaunga mkono watu wake na kumuua Mmisri. (Matendo 7:23, 24) Musa analazimika kukimbilia Midiani. Akiwa huko anaoa na kuwa mchungaji. Kwenye mti unaoteketea kimuujiza, Yehova amtuma Musa arudi Misri ili kuwaongoza Waisraeli watoke utumwani. Haruni, ndugu yake, achaguliwa kuwa msemaji wake.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha KutokaMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
MIUJIZA YA AJABU YALETA UKOMBOZI
Musa na Haruni wanasimama mbele ya Farao, wakimwomba awaruhusu Waisraeli waende kumfanyia Yehova sherehe nyikani. Mtawala huyo wa Misri anakataa katakata. Yehova anamtumia Musa kuleta mapigo makali moja baada ya lingine. Ni baada tu ya pigo la kumi kwamba Farao anawaruhusu Waisraeli waondoke. Hata hivyo, muda mfupi baadaye, Farao na jeshi lake wanawafuata mbio-mbio. Lakini Yehova anawafungulia watu wake njia katikati ya Bahari Nyekundu na kuwakomboa. Wamisri wanaowafuata wanakufa wakati maji ya bahari yanapowafunika.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha KutokaMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
YEHOVA APANGA TAIFA LA KITHEOKRASI
Miezi mitatu baada ya Waisraeli kukombolewa kutoka Misri, wanapiga kambi chini ya Mlima Sinai. Wakiwa huko wanapokea Amri Kumi na sheria nyingine, wanafanya agano pamoja na Yehova, na wanakuwa taifa la kitheokrasi. Musa anakaa siku 40 mlimani na kupokea maagizo kuhusu ibada ya kweli na ujenzi wa maskani ya Yehova, yaani, hekalu lenye kubebeka. Wakati huohuo, Waisraeli wanatengeneza na kuabudu ndama ya dhahabu. Anaposhuka kutoka mlimani, Musa anaona hayo na kukasirika sana hivi kwamba anavunja yale mabamba mawili ya mawe aliyopewa na Mungu. Baada ya wakosaji kuadhibiwa ifaavyo, Musa anapanda tena mlimani na kupewa mabamba mengine mawili. Anaporudi, ujenzi wa maskani unaanza. Mwishoni mwa mwaka wa kwanza wa Waisraeli wakiwa huru, hema hilo zuri na vitu vyote vilivyomo ndani vinakamilishwa na kupangwa. Kisha Yehova analijaza utukufu wake.
-