-
Wanyama wa Pori wa Dunia WanaotowekaAmkeni!—1997 | Julai 8
-
-
Hii ni kwa sababu usomapo makala hiihii, maelfu ya mimea na wanyama yanatoweka kwa kasi. Dakt. Edward O. Wilson, mwanabiolojia kwenye Chuo Kikuu cha Harvard, akadiria kwamba spishi 27,000 kwa mwaka, au spishi tatu kwa kila saa, hutoweka. Kwa kiwango hicho, kufikia asilimia 20 ya spishi za dunia zingeweza kutoweka katika miaka 30 ijayo. Lakini kutoweka hakudumu kwa kiwango kilekile; kunazidi kuongezeka. Inatabiriwa kwamba kufikia mwanzo-mwanzo wa karne ifuatayo, mamia ya spishi zitakuwa zikitoweka kila siku!
-
-
Wanyama wa Pori wa Dunia WanaotowekaAmkeni!—1997 | Julai 8
-
-
“Je, kutoweka kwa wanyama si utaratibu wa kiasili? Jibu ni la, angalau si kwa kiwango ambacho kutoweka kumetukia katika nyakati za majuzi. Kwa muda mrefu katika miaka 300 ambayo imepita, kiwango cha kutoweka kwa spishi kilikuwa karibu spishi moja kwa mwaka. Kwa sasa, kiwango cha kutoweka kunakosababishwa na wanadamu ni angalau mara elfu moja kuliko cha awali. . . . Kisababishi cha ongezeko hilo la kutoweka kwa wanyama ni utendaji wa kibinadamu.”—The New York Public Library Desk Reference.
-