-
Samoni wa Atlantiki Yumo HatariniAmkeni!—2004 | Desemba 8
-
-
Mahali hususa ambapo samoni walipata chakula hapakujulikana hadi kufikia miaka ya 1950, wakati wavuvi wanaouza samaki walipoanza kuvua samoni wengi kwenye ufuo wa Greenland. Mahali pengine kama hapo paligunduliwa karibu na Visiwa vya Faeroe, kaskazini mwa Scotland. Baadaye maeneo mengine kama hayo yaligunduliwa. Pia imeripotiwa kwamba samoni fulani hulisha chini ya barafu ya Aktiki! Maeneo hayo yalipogunduliwa, samoni wa Atlantiki walianza kukabili hatari kubwa. Viwanda vikubwa vya samaki vilijengwa huko Greenland na katika Visiwa vya Faeroe. Samaki wengi sana walivuliwa na wavuvi wanaouza samaki, na idadi ya samaki wanaorudi kwenye mito ili kuzalisha ikapungua sana. Serikali zilipotambua kwamba hilo ni tatizo kubwa, ziliwawekea wavuvi vikwazo. Hatua hiyo imewalinda samoni waliomo baharini.
-
-
Samoni wa Atlantiki Yumo HatariniAmkeni!—2004 | Desemba 8
-
-
Anapokuwa njiani, samoni hukabili magumu mengine kama vile mabwawa asiyoweza kupanda, mitambo ya nguvu za umeme, au vizuizi vingine vilivyojengwa na mwanadamu. Yeye hufanya nini anapokabili magumu hayo? Deirdre, mtafiti wa samoni, anasema: “Watu wengi wanaohangaikia kuhifadhiwa kwa samoni hutengeneza njia nyingine. Wao hutengeneza vidimbwi mbalimbali vinavyofuatana ili kuwawezesha samaki kuepuka kizuizi hicho kikubwa. Vidimbwi hivyo huitwa ngazi ya samaki au kivukio cha samaki. Kivukio hicho humwezesha samoni kuruka kwa usalama hadi kwenye kidimbwi kilicho juu anaposafiri kurudi kwenye eneo la kuzalisha.”
Deirdre anasema: “Hata hivyo, mbinu hiyo haifanikiwi nyakati zote.” Kisha anaongezea: “Nimeona samoni kadhaa wakiepuka vidimbwi hivyo. Wao hutambua tu njia waliyotumia awali nao hujitahidi kufa na kupona kuvuka kizuizi hicho kipya kilichotengenezwa na mwanadamu. Wengi wao hufa kwa sababu ya kuchoka sana au kujigonga kwenye kizuizi hicho.”
Maeneo ya Kufuga Samoni
Samoni ni chakula kinachofaidi mwili. Kwa sababu ya kupungua kwa samoni wa Atlantiki, samoni hufugwa katika maeneo fulani na kuuzwa. Samoni huhifadhiwa katika vyombo vyenye maji yasiyokuwa na chumvi ambavyo huwekwa ufuoni hadi wanapokua kufikia hatua ya smolt. Kisha wao huhamishiwa baharini kwenye vyombo vilivyo kama vizimba ambako wao hutunzwa hadi wanapokomaa na kuwa tayari kuuzwa kwenye mikahawa na maduka ya vyakula.
Samoni wanaofugwa kwa njia hiyo hukabili matatizo pia. Wafugaji wa samaki huwalisha chakula kilichotengenezewa viwandani. Hilo, pamoja na kufungiwa katika vizimba, hufanya samoni waathiriwe kwa urahisi na magonjwa na wadudu kama vile viroboto wa majini. Baadhi ya dawa zinazonyunyizwa ili kuwalinda ni hatari sana. Ernest, ambaye ni mpiga-mbizi, anasema: “Nilipokuwa nikiogelea chini ya maeneo ya kufugia samaki niliona kwamba hakukuwa na viumbe wowote katika maeneo hayo.”
Samoni wa Atlantiki Yumo Taabani
Samoni wengi hunaswa katika nyavu kabla ya kurudi kwenye mto walimozaliwa. Wavuvi fulani huwavua samoni kinyume cha sheria kwa sababu wana thamani kubwa. Samoni wachache wanaofaulu kurudi katika mto walimozaliwa huhatarishwa pia na wavuvi waliopewa kibali cha kuvua kwa ndoano. Ili kuwalinda samoni, hatua mbalimbali zimechukuliwa kama vile kuwaruhusu watu kuvua samaki katika maeneo hususa tu, kupandisha ada ya kupata leseni ya kuvua samoni, na kuwaruhusu watu kuvua samaki katika kipindi hususa. Hata hivyo, inakadiriwa kwamba samaki mmoja kati ya watano atanaswa anaporudi mtoni.
Isitoshe, samoni wasiofugwa hupata magonjwa, na hilo limepunguza sana idadi yao. Ugonjwa mmoja unaowakumba husababisha vidonda kwenye ngozi yao na mwishowe wanakufa. Pia uchafu unaotoka viwandani na dawa za kuua wadudu huingia kwenye mito na kuhatarisha samoni na viumbe wengine wa majini.
Unapofikiria hatari zote hizo anazokabili, si ajabu kwamba samoni yumo taabani. Anaendelea kukabili matatizo licha ya jitihada bora za mwanadamu. Viumbe wataacha kuangamizwa wakati ambapo Mungu Mweza-Yote, ambaye ni Muumba wa dunia, atakapowazuia wanadamu wasiiharibu dunia.—Isaya 11:9; 65:25.
-