Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Bado Inawezekana Kuwa na Imani ya Kweli?
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Oktoba 1
    • Imani Iliyopotea

      Watu wanaweza kupoteza imani waliyo nayo kwa sababu nyingi. Miongoni mwa sababu hizo ni mateso na majaribu ya kila siku. Kwa mfano, Profesa Michael Goulder, alikuwa kasisi wa parokia moja huko Manchester, Uingereza, wakati kulipotokea aksidenti ya ndege huko Munich mwaka wa 1958 ambapo wachezaji wengi wa timu ya soka ya Manchester United walikufa. Katika kipindi cha televisheni ya BBC, mtangazaji Joan Bakewell alieleza kwamba Goulder “alihisi akiwa hoi alipoona jinsi wanadamu wanavyoteseka.” Kwa sababu hiyo “alipoteza imani yake katika Mungu ambaye huingilia kati mambo yanayompata mwanadamu.” Goulder alisema kuwa anaamini kwamba “Biblia si . . . neno la Mungu lisilo na kosa” bali “ni neno la binadamu linaloweza kukosea, na labda ni sehemu fulani tu za Neno hilo ambazo zimepuliziwa na Mungu.”

      Nyakati fulani imani hufifia tu. Ndivyo ilivyotukia kwa mwandishi na mtangazaji Ludovic Kennedy. Anasema kwamba tangu utotoni alipatwa na shaka [kuhusu Mungu] mara kwa mara, akazidi kupoteza imani. Yaonekana hakuna mtu ambaye angeweza kujibu maswali yake kwa njia yenye kuridhisha. Imani yake ambayo tayari ilikuwa imedhoofika ilipata pigo kubwa sana babake alipokufa baharini. Sala kwa Mungu “atuhifadhi tusipatwe na hatari za baharini na jeuri ya adui” hazikujibiwa wakati meli ya kijeshi iliyogeuzwa kuwa ya abiria, ambamo baba yake alikuwa akisafiria, iliposhambuliwa na kuharibiwa na meli za kivita za Ujerumani wakati wa Vita ya Pili ya Ulimwengu.—All in the Mind—A Farewell to God.

  • Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Oktoba 1
    • Watu wengine huona imani hiyo kuwa ndoto tu. Ludovic Kennedy asema kwamba ‘watu wasio na uhakika huamini kwamba wakati wa maisha ya baada ya kifo kutakuwa na mlio wa mwisho wa tarumbeta, kutakuwa na maziwa na asali na kwamba mahali fulani huko Edeni watu watafurahia kuwa pamoja na wale waliokufa kabla yao na wengine ambao huenda wakafa baada yao.’ Kupatana na taarifa hiyo, lazima tuzushe swali la kuipinga, Ni jambo gani lililo la busara—kuamini kwamba “uzima ndio uu huu tu, kwa hiyo tuufurahie kadiri tuwezavyo,” kama adokezavyo Kennedy, au tuamini Mungu na ahadi yake ya ufufuo? Sarah Jayne aliamua kumwamini Mungu na ahadi yake ya ufufuo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki