Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Basi, wakati wa hukumu “kuanza na nyumba ya Mungu” ulipofika mwaka wa 1918, Yehova aliiondoa Jumuiya ya Wakristo. Msimamizi-nyumba mwingine aliteuliwa—“msimamizi-nyumba mwaminifu, mwenye busara”—na kuwekwa rasmi juu ya nyumba ya Yesu duniani. (1 Petro 4:17; Luka 12:42-44) Jamii hiyo yenye washiriki wengi imejithibitisha yenyewe kuwa yastahili kubeba “ufunguo” wa kifalme wa nyumba ya Daudi. Sawa na “msumari” unaotumainika, imethibitika kuwa muungaji mkono anayetegemeka kwa ajili ya “vyombo” vyote mbalimbali, Wakristo watiwa-mafuta walio na wajibu mbalimbali wanaoitegemea iwaruzuku kiroho. “Kondoo wengine” pia, kama ‘mgeni aliye katika malango’ ya Yerusalemu la kale, huutegemea “msumari” huo, Eliakimu wa leo.—Yohana 10:16; Kumbukumbu la Torati 5:14.

      22. (a) Kwa nini kuchukuliwa kwa mahali pa Shebna akiwa msimamizi-nyumba kulikuwa kwa wakati unaofaa? (b) Katika nyakati za kisasa, kwa nini kuwekwa rasmi kwa “msimamizi-nyumba mwaminifu, mwenye busara,” kulikuwa kwa wakati unaofaa?

      22 Eliakimu alichukua mahali pa Shebna wakati ambapo Senakeribu na majeshi yake walikuwa wakitisha Yerusalemu. Vivyo hivyo, “msimamizi-nyumba mwaminifu, mwenye busara,” amewekwa rasmi kutumikia wakati wa mwisho, ambao utafikia kikomo Shetani na majeshi yake wajapo kushambulia mara ya mwisho “Israeli wa Mungu” na waandamani wao wa kondoo wengine. (Wagalatia 6:16) Kama ilivyokuwa katika siku ya Hezekia, shambulio hilo litaishia kwenye kuharibiwa kwa adui za uadilifu. Wale wanaoegemea kwenye “msumari mahali palipo imara,” msimamizi-nyumba mwaminifu, wataokoka, kama vile tu wakazi waaminifu wa Yerusalemu walivyookoka uvamizi wa Ashuru dhidi ya Yuda.

  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Yehova aeleza kupitia Isaya: “Itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nyumba ya Yuda. Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.” (Isaya 22:20-22) Eliakimu, atakayechukua mahali pa Shebna, atapewa mavazi rasmi ya msimamizi-nyumba huyo pamoja na ufunguo wa nyumba ya Daudi. Biblia hufananisha “ufunguo” na mamlaka, serikali, au uwezo. (Linganisha Mathayo 16:19.) Nyakati za kale, mshauri wa mfalme, aliyekabidhiwa funguo, angeweza kusimamia kwa jumla nyumba za mfalme, hata kutoa uamuzi juu ya wale wanaoteuliwa katika utumishi wa mfalme. (Linganisha Ufunuo 3:7, 8.) Basi, ofisi ya msimamizi-nyumba ni muhimu, na yeyote anayetumikia humo hutarajiwa kufanya mengi. (Luka 12:48)

  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 19, 20. (a) Eliakimu atathibitikaje kuwa baraka kwa watu wake? (b) Ni nini kitakachowapata wale wanaoendelea kumtegemea Shebna?

      19 Hatimaye, Yehova atumia mfano kueleza kuhamishwa kwa mamlaka kutoka kwa Shebna hadi kwa Eliakimu. Ataarifu hivi: “Nitamkaza [Eliakimu] kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake. Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia. Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari [Shebna] uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.”—Isaya 22:23-25.

      20 Katika mistari hiyo msumari wa kwanza ni Eliakimu. Atakuwa “kiti cha utukufu” kwa nyumba ya baba yake, Hilkia. Tofauti na Shebna, hataiaibisha nyumba ya baba yake wala sifa yake. Eliakimu atakuwa tegemeo lenye kudumu kwa vyombo vya nyumbani, yaani, kwa wengine walio katika utumishi wa mfalme. (2 Timotheo 2:20, 21)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki