Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 1. (a) Yohana anatendaje kama itikio anapoona kahaba mkubwa na mpandwaji wake mwenye kutia hofu, na kwa nini? (b) Jamii ya Yohana inatendaje leo kama itikio, matukio yanapokunjuka katika utimizo wa njozi ya kiunabii?

      TENDO-MWITIKIO la Yohana ni nini anapomwona “kahaba mkubwa” na mpandwaji wake mwenye kutia hofu? Yeye mwenyewe ajibu: “Basi, nilipoona yeye mimi nilistaajabu kwa staajabu kubwa.” (Ufunuo 17:6b, NW) Mawazo vivi hivi tu ya kibinadamu hayangeweza kutunga mwono kama huo. Hata hivyo ndio huo—mbali kule jangwani—malaya mpujufu akimpanda hayawani-mwitu wa kutisha mwenye rangi-damu-nyangavu! (Ufunuo 17:3) Jamii ya Yohana leo pia hustaajabu kwa staajabu kubwa matukio yanapokunjuka katika utimizo wa njozi ya kiunabii.

  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 2. (a) Katika kuitikia mshangao mkubwa wa Yohana, malaika anamwambia nini? (b) Jamii ya Yohana imefunuliwa nini, na hilo limefanywaje?

      2 Malaika anaona mshangao mkubwa wa Yohana. “Na hivyo,” Yohana aendelea, “malaika akasema kwa mimi: ‘Kwa nini wewe ulistaajabu? Mimi nitakuambia fumbo la mwanamke na la hayawani-mwitu ambaye anabeba yeye na ambaye ana vichwa saba na pembe kumi.’” (Ufunuo 17:7, NW) Aha, sasa malaika atalifumbua fumbo! Yeye amfafanulia Yohana mwenye kukodoa macho nyuso mbalimbali za njozi na matukio ya kidrama yanayokaribia kukunjuka. Hali kadhalika, inapotumikia chini ya mwelekezo wa kimalaika leo, jamiii ya Yohana yenye kutazama imefunuliwa uelewevu wa huo unabii. Je! “kufasiri si kazi ya Mungu?” Kama Yosefu mwaminifu, sisi tunaitikadi kwamba ni yake. (Mwanzo 40:8; linga Danieli 2:29, 30.) Watu wa Mungu wamewekwa kana kwamba wako katikati ya jukwaa, Yehova anapowafasiria maana ya njozi na matokeo yayo juu ya maisha zao. (Zaburi 25:14) Kwa wakati barabara, yeye amewafungulia uelewevu wao fumbo la mwanamke na hayawani-mwitu.—Zaburi 32:8.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki