-
Kilimo cha Kisasa Kimebadili UlimwenguAmkeni!—2009 | Septemba
-
-
Wakulima Bado Wakabili Matatizo
Katika nchi zenye utajiri, bado wakulima wengi wanalazimishwa kuyaacha mashamba yao kwa kuwa hawawezi kushindana na mashirika makubwa ya kilimo. Wakulima fulani wanaweza tu kuendelea kuishi maisha ya kawaida kwa kugeuza mashamba yao kuwa mahali pa tafrija kutia ndani kujenga vyumba vya kukodi watalii au kuwa viwanja vya kupigia kambi, kucheza gofu, na kutokeza sanaa. Wengine huanza kukuza mazao ya pekee kama vile chakula kilichokuzwa kwa mbolea ya kiasili, maua, na kufuga mbuni, na alpaca.
Katika nchi maskini, ambako asilimia 80 hivi ya idadi ya watu wanapata riziki yao kwa kukuza mazao yao, wakulima wengi pia wanakumbwa na badiliko kubwa. Kampuni za kimataifa zinazotumia mbinu za kulima mashamba makubwa zinaweza kununua mashamba bora zaidi na kukuza mimea itakayouzwa katika nchi za mbali. Kwa upande ule mwingine, wakulima wadogo-wadogo hulima mashamba madogo sana au yasiyo na rutuba mara nyingi bila kutumia mashini ili waandalie familia zao chakula.
-
-
Kilimo cha Kisasa Kimebadili UlimwenguAmkeni!—2009 | Septemba
-
-
Lakini ninategemea sana mashini hizo, na jambo hilo ndilo husababisha mkazo. Mara kwa mara ninalazimika kukopa pesa ili kununua mashini nyingine. Kulipa mkopo huo kunategemea mambo ambayo siwezi kuyadhibiti kama vile, mvua, baridi kali, bei ya bidhaa sokoni, na riba ambayo benki itanitoza. Mkazo unaotokezwa na ukulima umesababisha matatizo mengi katika ndoa katika eneo hili, na hata kujiua.”
-