Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Mfungo Ni Jambo la Kale?
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 15
    • NIMEKUWA nikifunga kila Jumatatu tangu nilipokuwa tineja,” asema Mrudulaben, mwanamke Mhindi aliyefana mwenye umri wa miaka 78. Mfungo umekuwa sehemu ya ibada yake, njia ya kuhakikisha kwamba alikuwa na ndoa nzuri na watoto wenye afya, na vilevile ulinzi kwa ajili ya mumewe. Sasa akiwa mjane, yeye huendelea kufunga siku za Jumatatu kwa ajili ya afya njema, na kwa ajili ya ufanisi wa watoto wake. Sawa na yeye, wanawake Wahindu walio wengi hufanya mifungo ya ukawaida iwe sehemu ya maisha yao.

      Prakash, mfanyabiashara wa makamo anayeishi katika kiunga cha Mumbai (Bombay), India, asema kwamba yeye hufunga kila mwaka kwenye Jumatatu za Sawan (Shravan). Huo ni mwezi wenye umaana wa pekee wa kidini kwenye kalenda ya Kihindu. Prakash aeleza hivi: “Nilianza kufunga kwa sababu za kidini, lakini sasa napata kichocheo cha ziada cha kuendelea kwa sababu za kiafya. Kwa kuwa Sawan huja kuelekea mwishoni mwa kuvuma kwa upepo wa monsuni, mfungo huupa mwili wangu fursa ya kuondolea mbali magonjwa ya kawaida ya msimu wa mvua.”

  • Je, Mfungo Ni Jambo la Kale?
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 15
    • Mfungo ni desturi maarufu katika Dini ya Hindu. Siku fulani-fulani, chasema kitabu Fast and Festivals of India, “watu hufunga kabisa . . . hata maji hayanywewi hata kidogo. Wanaume na pia wanawake hufunga kabisa-kabisa . . . ili kuhakikisha kuna furaha, ufanisi na msamaha wa ukiukaji-sheria na dhambi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki