-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Mnamo 1716, Mwingereza fulani alipata leseni ya kukamua mafuta ya alizeti na kuyatumia katika kiwanda cha kufuma na kulainisha ngozi. Hata hivyo, watu katika maeneo mengi huko Ulaya hawakujua chochote kuhusu mafuta hayo hadi miaka ya 1800. Ama kweli, Maliki Petro Mkuu wa Urusi ndiye aliyetoa mbegu za alizeti huko Uholanzi katika mwaka wa 1698 na kuzipeleka Urusi. Hata hivyo, uzalishaji na uuzaji wa alizeti ulianza muda mrefu baadaye katika miaka ya 1830. Miaka michache baadaye, katika eneo la Voronezh huko Urusi, maelfu ya tani za mafuta ya alizeti yalikuwa yakitengenezwa. Muda si muda, maua ya alizeti yalipandwa katika maeneo jirani ya Bulgaria, Hungary, Rumania, Ukrainia na nchi ambayo zamani iliitwa Yugoslavia.
-
-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Ni jamii mbili tu ambazo huzalishwa. Jamii moja ni Helianthus annuus, ambayo hupandwa hasa ili kutokeza mafuta ya alizeti.
-
-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Leo, alizeti hupandwa kwa wingi hasa kwa sababu mbegu zake hutokeza mafuta bora. Mafuta ya alizeti hutumiwa katika upishi, katika saladi, na kutengeneza siagi.
-
-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Isitoshe, mafuta ya alizeti hutumiwa kutengeneza sabuni za nywele, dawa ya kujipaka midomo inapokauka, mafuta ya kujipaka, na bidhaa za watoto. Hutumiwa pia viwandani kutengeneza mafuta ya magari na mashine nyinginezo.
-