Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Familia Zisizo na Baba Ni Tatizo Linaloongezeka
    Amkeni!—2004 | Agosti 22
    • Akina Baba Wasiotimiza Madaraka Yao

      Tafadhali ona sanduku “Baba, Utarudi Lini?” Nao, ambaye sasa ana umri wa miaka 23, anakubali hivi: “Nilimwona Baba mara chache sana kabla ya kuingia shule ya msingi. Siku moja alipokuwa akiondoka nyumbani, nilimsihi hivi, ‘Tafadhali usikose kurudi.’”

      Mahusiano ya familia kama yale ya Nao na baba yake ndiyo yaliyomchochea Piotr Szczukiewicz, mwandishi kutoka Poland, kusema hivi: “Yaelekea baba ndiye mtu muhimu anayekosekana katika familia.” Ni kweli kwamba baba wengi huishi na familia zao na kuzitegemeza kiuchumi. Hata hivyo, kama vile gazeti Capital la Ufaransa lilivyoeleza, “baba wengi huridhika tu na kuandalia familia zao chakula huku wakipuuza kuwafundisha watoto wao.”

      Mara nyingi kuna baba katika familia, lakini hajihusishi na maisha ya watoto wake. Anahangaikia mambo mengine. Jarida Famille chrétienne la Ufaransa linasema hivi: “[Baba] anaweza kuwepo kihalisi, lakini huenda asiwepo kiakili.” Kwa nini leo baba wengi wamejitenga na familia zao kiakili na kihisia?

      Kulingana na jarida hilo, sababu kuu ni kwamba “yeye hukosa kuelewa daraka lake akiwa baba au mume.” Kulingana na maoni ya baba wengi, daraka la baba mzuri ni kuleta mshahara mnono. Kama alivyosema mwandishi Józef Augustyn, kutoka Poland, “baba wengi hufikiri wao ni wazazi bora kwa sababu wanachuma pesa kwa ajili ya familia.” Lakini hilo ni mojawapo tu ya madaraka ya baba.

      Ukweli ni kwamba watoto hawawathamini baba zao kulingana na kiasi cha pesa wanazochuma au thamani ya zawadi wanazowapatia. Badala yake, watoto hutaka hasa upendo, wakati, na uangalifu kutoka kwa baba wala si zawadi. Hayo ndiyo mambo muhimu kwao.

      Baba Wanahitaji Kujichunguza

      Kulingana na ripoti ya Baraza Kuu la Elimu la Japani, “akina baba wanapaswa kuchunguza maisha yao kwa sababu wanatumia wakati mwingi kazini.” Swali ni, Je, baba yuko tayari kufanya marekebisho kwa faida ya watoto wake? Gazeti la Ujerumani Gießener Allgemeine, liliripoti uchunguzi fulani ulioonyesha kwamba baba wengi walikataa kuwatanguliza watoto wao badala ya kazi yao.

      Watoto wanaweza kuumia sana kihisia wanapoona kwamba baba hawajali. Lidia, ambaye sasa ana umri wa miaka 21, anakumbuka vizuri jinsi baba yake alivyokuwa akifanya alipokuwa msichana mdogo huko Poland. Anasema: “Hakuzungumza nasi hata kidogo. Maisha yetu yalitofautiana kabisa. Hakujua kwamba nilikuwa nikienda disko.” Vilevile Macarena, msichana mwenye umri wa miaka 21 huko Hispania, anasema kwamba alipokuwa mtoto, baba yake “alizoea kwenda kujifurahisha na marafiki zake mwishoni mwa juma, na mara kwa mara hakurudi nyumbani kwa siku kadhaa.”

  • Familia Zisizo na Baba Ni Tatizo Linaloongezeka
    Amkeni!—2004 | Agosti 22
    • [Sanduku katika ukurasa wa 3]

      “Baba, Utarudi Lini?”

      Hilo ndilo swali ambalo Nao, msichana Mjapani mwenye umri wa miaka mitano, alimwuliza baba yake alipokuwa akienda kazini siku moja. Ingawa aliishi nyumbani, Nao alimwona mara chache sana. Kwa kawaida alifika nyumbani Nao akiwa amelala na kwenda kazini kabla hajaamka.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki