-
Tamaa ya Kusafiri Salama kwa NdegeAmkeni!—2002 | Desemba 8
-
-
Tamaa ya Kusafiri Salama kwa Ndege
MAJUMA machache tu kabla ya Septemba 11, 2001, Alex aliona kuwa yuko karibu kushinda woga wake wa kusafiri kwa ndege. Ndege ya abiria ilipokuwa ikianza safari toka Athens kwenda Boston, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 42 ambaye ni meneja wa uhusiano mwema katika kampuni yao alianza kuwa na wasiwasi—moyo wake ulianza kupiga kwa nguvu na mikono yake na uso wake ukajaa jasho.
Lakini alijua kile alichopaswa kufanya. Mwalimu wake aliyekuwa akimsaidia kushinda woga wa kusafiri kwa ndege alikuwa amemwambia kwamba anapaswa kuvuta pumzi, kuwazia mandhari yenye kupendeza, na kushikilia kiti kwa nguvu, na kukiachilia mara nne kila dakika. Alipobabaishwa na mitikiso na makelele ya ndege, Alex aliwazia yuko kwenye pwani tulivu. Alex alisema: “Nilidhani kwamba nimefaulu sana kushinda woga wangu.”
Mamilioni ya abiria wameogopa kusafiri kwa ndege. Katika miaka ya hivi majuzi, wengi wameshauriwa na watu wa familia, waajiri, na mashirika ya ndege waende kwenye shule za kuwasaidia watu kushinda woga wa kusafiri kwa ndege. Abiria wengi walifanya maendeleo makubwa baada ya kuhudhuria mafunzo hayo, na katika vituo vingi asilimia 90 ya waliohudhuria mafunzo hayo walifaulu kushinda woga wa kusafiri kwa ndege.
Lakini matukio ya Septemba 11, 2001 yaliharibu mafanikio hayo. Alex aliacha kuhudhuria mafunzo hayo mara moja. Na mwajiri wake alihuzunika sana wakati Alex alipovunja mpango wa kusafiri kwa ndege ili akutane na mtu mmoja mashuhuri ambaye angekuwa mteja wao. Alex alisema hivi: “Singeweza kustahimili woga wangu wa kusafiri kwa ndege pamoja na mashambulizi ya magaidi. Mafunzo niliyopata hayakunitayarisha kukabili mambo hayo.”
-
-
Tamaa ya Kusafiri Salama kwa NdegeAmkeni!—2002 | Desemba 8
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 5]
Mambo Fulani Kuhusu Usafiri wa Ndege
Kulingana na makadirio fulani, asilimia 20 ya abiria huogopa kusafiri kwa ndege. Hata hivyo, si wote wanaona kwamba kusafiri kwa ndege ni hatari. Mara nyingi, wasiwasi wao husababishwa na mambo mengine wanayoogopa kama vile kuwa mahali palipo juu sana au katika sehemu zenye watu wengi.
-