Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jihadhari Na Mitego Ya Ibilisi!
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • 10. Ni nini kilichomfanya Petro amkane Kristo?

      10 Mtume Petro alikuwa kati ya marafiki wa karibu zaidi wa Yesu. Alitangaza hadharani kwamba Yesu alikuwa ndiye Masihi. (Mt. 16:16) Petro alibaki mshikamanifu wakati wanafunzi wengine walipokosa kuelewa maana ya yale ambayo Yesu alisema na hivyo wakamwacha. (Yoh. 6:66-69) Na maadui walipokuja kumkamata Yesu, Petro aliutumia upanga kumlinda Bwana wake. (Yoh. 18:10, 11) Hata hivyo, baadaye Petro alishindwa na woga na kukana kwamba hata hamjui Yesu Kristo. Kwa kipindi fulani, mtume huyo alinaswa katika mtego wa kuogopa wanadamu na akaruhusu woga huo umzuie kuwa jasiri.​—Mt. 26:74, 75.

  • Jihadhari Na Mitego Ya Ibilisi!
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 15
    • Petro alikuwa na ujuzi sahihi na pia alimpenda Mungu. Hata hivyo, nyakati nyingine alikosa sifa ya kiasi, akawa mwoga, na akashindwa na msongo wa watu. Kabla ya Yesu kukamatwa, Petro alijigamba hivi: “Hata ikiwa wengine wote watakwazika, hata hivyo mimi sitakwazika.” (Marko 14:29) Mtume huyo angejitayarisha vizuri zaidi kukabiliana na majaribu yaliyokuwa mbele yake ikiwa angekuwa na msimamo kama ule wa mtunga-zaburi aliyemtegemea Mungu na kuimba hivi: “Yehova yuko upande wangu; sitaogopa. Mtu wa udongo anaweza kunitenda nini?” (Zab. 118:6) Usiku wa mwisho wa maisha Yake duniani, Yesu alimchukua Petro na mitume wengine wawili na kuingia ndani kabisa ya bustani ya Gethsemane. Hata hivyo, badala ya kukaa macho, Petro na wenzake walilala usingizi. Yesu aliwaamsha na kusema: “Endeleeni kukesha na kusali, ili msiingie katika jaribu.” (Marko 14:38) Lakini Petro alilala tena na baadaye akashindwa na woga na pia msongo wa watu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki