Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Elekea Mahali Ilipo Nuru
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
    • Karibu na Nchi ya Ahadi

      Chini ya uongozi wa Musa, Waisraeli waliweza kukimbia kutoka Misri. Muda si muda, walikaribia mpaka wa kusini wa Nchi ya Ahadi. Musa akawatuma wanaume 12 ili waipeleleze nchi. Wapelelezi kumi ambao hawakuwa na imani walileta ripoti mbaya, wakisema kwamba Waisraeli hawangeweza kuwashinda Wakanaani kwa sababu walikuwa “wenye ukubwa usio wa kawaida” na wenye nguvu zaidi kijeshi. Hilo lilikuwa na matokeo gani kwa Waisraeli? Masimulizi hayo yanatuambia kwamba walianza kunung’unika juu ya Musa na Haruni, wakisema: “Kwa nini Yehova anatuleta kwenye nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu wadogo watakuwa nyara. . . . Na tuchague kiongozi, nasi turudi Misri!”—Hesabu 13:1, 2, 28-32; 14:1-4.

  • Elekea Mahali Ilipo Nuru
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
    • Katika jitihada zake za mwisho za kujaribu kuwazuia watumishi wa leo wa Yehova wasipate thawabu yao, Shetani hahitaji mbinu mpya. Akitumia mbinu inayotukumbusha yaliyotukia wakati Waisraeli walipokaribia Nchi ya Ahadi kwa mara ya kwanza, mara nyingi Shetani anajaribu kutufanya tuogope na kuwa na shaka, iwe ni kupitia vitisho, mateso, au dhihaka. Wakristo fulani wameshindwa na vitisho hivyo. (Mathayo 13:20, 21)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki