-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
8. Yesu apataje furaha katika kumcha Yehova?
8 Mesiya anamchaje Yehova? Kwa hakika, Yesu hatishwi na Mungu, akihofu hukumu yake. Badala yake, Mesiya anamcha Mungu kwa staha, staha yenye upendo kwake. Mtu mwenye kumhofu Mungu hutamani ‘kufanya sikuzote mambo yale yanayompendeza,’ kama afanyavyo Yesu. (Yohana 8:29) Kwa neno na tendo, Yesu afundisha kwamba hakuna shangwe kubwa zaidi kuliko ile inayotokana na kutembea kila siku katika hofu ifaayo ya Yehova.
-
-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
6. Yatabiriwa kwamba Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani?
6 Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani? Je, atakuwa kama Mwashuri mkatili, mshupavu, anayeharibu ufalme wa kaskazini wa Israeli wenye makabila kumi? Sivyo hata kidogo. Isaya asema hivi kumhusu Mesiya: “Roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA.” (Isaya 11:2, 3a)
-