Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuwatazama Wasikilizaji
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Unapofanya hivyo, jaribu kumtazama macho mtu huyo—au angalau mtazame usoni kwa heshima na fadhili. Tabasamu changamfu ya mtu mwenye shangwe ya moyoni huvutia sana. Tabasamu kama hiyo inaweza kumwonyesha wewe ni mtu wa aina gani na kumfanya astarehe zaidi mnapozungumza.

  • Kuwatazama Wasikilizaji
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Iwe unahubiri au unaongoza funzo la Biblia la nyumbani, jaribu kumtazama kwa heshima mtu unayezungumza naye. Lakini, usimkodolee macho kwani anaweza kuona haya. (2 Fal. 8:11) Lakini kwa njia ya kawaida na ya urafiki, mtazame mtu huyo usoni pindi kwa pindi. Katika nchi nyingi, kufanya hivyo huonyesha kwamba kwa kweli unapendezwa naye.

  • Kuwatazama Wasikilizaji
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Watu wengine wanaweza kukata kauli juu yetu na juu ya mambo tunayosema ikitegemea mahali tunapotazama. Katika jamii nyingi, watu huelekea kumtumaini mtu anayewatazama macho kwa njia ya kirafiki. Kwa upande mwingine, ikiwa mtu anatazama miguu yake tu au vitu vingine badala ya kumtazama mtu anayeongea naye, watu wanaweza kuwa na shaka iwapo anasema kweli au wanaweza kutilia shaka uwezo wake. Na katika jamii nyingine, kumtazama sana mtu mwingine kwa macho kunaonwa kuwa ufidhuli, uchokozi, au ukaidi. Ndivyo ilivyo hasa unapoongea na mtu wa jinsia tofauti au mkuu fulani au mtu yeyote mwenye mamlaka. Na katika maeneo mengine, ni kukosa adabu ikiwa mtu mwenye umri mdogo atazama macho ya mtu mwenye umri mkubwa wanapoongea.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki