-
‘Tumefanya Lile Tulilopaswa Kufanya’Mnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
Baada ya kuwa katika huduma ya nyumba hadi nyumba asubuhi, mwenzangu alitoa vipande viwili vya mkate. tulipomaliza kula, nilitoa sigareti ili nivute. “Umekuwa katika kweli kwa muda gani?” akaniuliza. “Nilihudhuria mkutano wa kwanza usiku uliopita,” Nikamjibu.
-
-
‘Tumefanya Lile Tulilopaswa Kufanya’Mnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
Katika 1938, miaka michache baadaye, postikadi ilipelekewa wale waliokuwa wameandikisha gazeti la Mnara wa Mlinzi ikiwaalika wahudhurie mkutano wa pekee katika nyumba ya faragha iliyokuwa umbali wa kilometa 25 hivi. Mama alitaka kuhudhuria, kwa hiyo Fern nami na ndugu zangu wawili tuliandamana naye. Waangalizi wasafirio wa Mashahidi wa Yehova, John Booth na Charles Hessler, walitutolea hotuba tukiwa watu 12 hivi. Baadaye, walianza kupanga ili kikundi fulani kishiriki katika huduma ya shambani asubuhi iliyofuata. Hakuna yeyote aliyejitolea kwenda nao, kwa hiyo Ndugu Hessler alinichagua na kuniuliza, “Kwa nini usiende nasi?” Sikujua kabisa walichokuwa wakienda kufanya, lakini sikuwa na sababu ya kutowasaidia.
Tulienda nyumba hadi nyumba hadi kipindi cha adhuhuri hivi, kisha Ndugu Hessler akatoa vipande viwili vya mkate. Tuliketi kwenye vipandio vya kanisa na kuanza kula. Ilikuwa baada ya kutoa sigara hiyo kwamba Ndugu Hessler alipata kujua kwamba nilikuwa nimehudhuria mkutano mara moja tu.
-