Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutana na Makabila ya Milimani ya Thailand
    Amkeni!—2010 | Mei
    • Jawlay, wa kabila la Lahu, anasema hivi: “Kufikia wakati nilipooa nikiwa na umri wa miaka 19, nilikuwa mlevi na mraibu wa dawa za kulevya. Singeweza kufanya kazi bila kutumia dawa za kulevya, na bila kufanya kazi sikuwa na pesa. Mke wangu, Anothai, alijihisi akiwa mpweke na hapendwi. Tulibishana kila wakati.

      “Binti yetu, Suphawadee, alipozaliwa, Anothai alianza kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova. Lakini mimi ningekimbilia msituni kila mara Mashahidi walipokuja nyumbani. Hata hivyo, mwenendo wa mke wangu ulianza kubadilika na kuwa mzuri. Alizungumza nami kwa heshima na alishughulikia majukumu yake nyumbani kwa njia nzuri zaidi. Kwa hiyo, aliponitia moyo nijifunze Biblia, nilikubali.

      “Mafundisho ya Biblia yaliponigusa moyo, nilifanya maendeleo hatua kwa hatua. Mwishowe, kwa msaada wa Mungu, nilishinda uraibu wangu. Sasa familia yangu ina furaha ya kweli kwa kuwa tumepata njia bora zaidi ya maisha! Pia tunafurahi kuwaeleza kweli za Biblia watu wengine wa makabila ya milimani.”

  • Kutana na Makabila ya Milimani ya Thailand
    Amkeni!—2010 | Mei
    • [Picha katika ukurasa wa 17]

      Jawlay akiwa na familia yake

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki