Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuna Uhitaji Mkubwa wa Faraja!
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
    • Kwa mfano, ebu mfikirie Svetlana, msichana mmoja wa nchi za Balkan aliyezaliwa katika familia fukara.b “Ili tupate pesa,” yeye asema, “nilikuwa nikitumwa na wazazi wangu kuomba-omba au kuiba. Maisha ya familia yetu yaliharibika sana kiasi cha kwamba nilishikwa kinguvu na mtu wa jamaa yetu. Nilipata kazi ya kuhudumu katika hoteli, na mama yangu, ambaye alikuwa akipokea mshahara wangu, alisema kwamba atajiua nikipoteza kazi hiyo. Hayo yote yakanitumbukiza katika maisha ya ukahaba. Nilikuwa na umri wa miaka 13 tu wakati huo. Nikashika mimba na kuitoa. Nilipokuwa na umri wa miaka 15, ungalidhani nina umri wa miaka 30.”

  • Farijiwa na Nguvu za Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
    • Svetlana, yule kahaba mdogo aliyetajwa katika makala iliyotangulia, alifarijiwa sana alipotambua kwamba Yehova anapendezwa naye binafsi. Mashahidi wa Yehova walimpata alipokuwa karibu kujiua. Kisha akakubali funzo la Biblia, ambalo lilimsaidia kumfahamu Yehova akiwa mtu halisi ambaye anapendezwa na hali njema yake. Jambo hilo lilimgusa moyo na kumchochea abadili maisha yake na kujiweka wakfu kwa Mungu. Pia lilimfanya Svetlana ajiheshimu na kumsaidia kuvumilia na kuwa na mtazamo mzuri maishani licha ya matatizo yake. “Nina hakika,” yeye asema sasa, “kwamba Yehova hataniacha kamwe. Nimeona ukweli wa maneno ya 1 Petro 5:7. Andiko hilo linasema: ‘Tupeni hangaiko lenu lote juu [ya Yehova], kwa sababu yeye huwajali nyinyi.’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki