Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Fiji

      Katika eneo fulani la mashambani, mapainia wanasafiri kwa miguu wanapohubiri, na njia wanazopitia zina vumbi au matope. Nagamma na binti yake, Reshma, ambao ni mapainia wa kawaida, walimwalika Ushla ambaye ni dada kipofu, aandamane nao na kufanya upainia kwa mwezi mmoja. Walitembea kwa kilomita nyingi kila siku wakiwa wamemshika mikono. Familia moja iliyokuwa imeketi nje ya nyumba yao siku moja yenye joto, walitazama dada hao watatu wakijaribu kuepuka kuingia kwenye vidimbwi vidogo kwenye barabara yenye matope. Kisha wakamwona yule dada kipofu akiingia kwenye kidimbwi na kujirushia matope kwenye mguu. Dada hao wengine walisimama na kumpangusa. Akitaka sana kujua yaliyokuwa yakiendelea, baba wa familia hiyo aliwaita dada hao. Alisema: “Kila siku tunawaona nyinyi watatu mkitembea. Mnaenda wapi?” Walimweleza kwamba walikuwa wakienda kuongoza funzo la Biblia. Mtu huyo aliwaambia kwamba ikiwa ujumbe wao ni muhimu sana hivi kwamba wanaenda mbali hivyo ili kuwafundisha watu, angependa kuusikia pia! Familia hiyo ilianza kujifunza.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 63]

      Nagamma na Reshma wakimsaidia Ushla

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki